Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa
akisalimiana na mdogo wa marehemu Betty Ndejembi, Aisha Ndejembi
aliyeuawa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mzee
Pancras Ndejembi na Mama Ndejembi ambao marehemu alikuwa mjukuu wao.Mh
Lowassa alikwenda nyumbani kwa mwanasiasa huyo mkongwe eneo la Uzunguni
mjini Dodoma kumpa pole ya kufiwa na mjukuu wake huyo.
Mzee Ndejembi akimuelezea Mh Lowassa mkasa mzima wa kifo Cha mjukuu
wake, Betty Ndejembi aliyeuawa jijini dar es salaam na watu
wasiyojulikana.
0 comments:
Post a Comment