Bi. Erasma Rutachura,
ambaye amepata ufadhili wa masomo nchini China,ngazi ya shahada ya uzamivu katika
mafuta na gesi akipokea nyaraka zitakazomwezesha kujiunga na masomo yake mwaka
huu.Anayempa nyaraka hizo ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (wa pili kutoka kulia).Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya
Nishati na Madini, Eliakim Maswi.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim
Maswi (wa tano kutoka kushoto waliosimama), akiwatambulisha wanafunzi waliopata
ufadhili wa masomo nchini China
Watanzania waliopata
ufadhili wa masomo nchini China katika ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu katika
fani ya mafuta na gesi wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini, Eliakim Maswi (wa nne kutoka kushoto mstari wa nyuma) pamoja na
watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kuagwa rasmi katika
Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.Wengine katika picha (mstari wa mbele) ni Kamishna Msadizi Nishati
anayeshughulikia Umeme, Eng.Innocent Luoga (wa kwanza kulia), Kamishna wa
Madini, Eng.Paul Masanja (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi Utawala - Bi.
Caroline Musika (wa kwanza kushoto).
*********
Serikali
ya China kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetoa ufadhili wa nafasi kumi
(10) za masomo kwa watanzania katika
ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi.
Katika
shahada ya uzamili wamechaguliwa watanzania 9 kati ya 46 walioomba ufadhili
ambapo katika shahada ya uzamivu amechaguliwa mtanzania mmoja kati ya wanne
waliowasilisha maombi.
Msaada huu wa masomo
umetolewa na Serikali ya China kwa Tanzania kufuatia juhudi za Wizara ya
Nishati na Madini kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa na rasilimaliwatu ya
kutosha katika kusimamia Sekta za Nishati na Madini hasa sekta ndogo ya mafuta
na gesi inayokua kwa kasi hapa nchini.
Ufadhili huu ni wa
pili kupitia Wizara ya Nishati na Madini ambapo wa kwanza ulitolewa katika
mwaka wa fedha 2013/14 kwa nafasi 10
katika ngazi ya shahada ya uzamili kwenye fani za nishati na madini ikiwemo
uhandisi migodi, uhandisi wa nishati katika mafuta na gesi. Wanafunzi hao
wanatarajia kuingia mwaka wa pili wa masomo mwezi septemba, 2014.
Nafasi hizi
zimepatikana kwa ushindani baada ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari ambapo
vigezo vilivyotumika kupata ufadhili ni aina ya kozi aliyoisoma mwombaji katika Shahada ya kwanza au Uzamili, Chuo alichosoma shahada ya kwanza, kiwango cha ufaulu katika shahada ya
kwanza kuanzia GPA 3.0 na Uwiano wa jinsia.
Faida ambazo Tanzania
itapata kutokana na ufadhili huu ni kuongeza wataalam katika fani za sekta za
nishati na madini na hasa sekta ndogo ya mafuta na gesi, kuongeza fursa za
masomo kwa watanzania hasa kwa kuzingatia kuwa wengi hukosa elimu kutokana na
kutomudu gharama, na kuzidi kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania
na China.
0 comments:
Post a Comment