Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (wa pili kushoto), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso, baada ya kuzindua warsha ya siku mbili ya Nishati ya mbadala kwa wadau wa Mawasiliano ya simu ya GSMA, inayofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja wa Programu wa GSMA Mobile, Ferdous Mottakin na Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa Towers Services Ltd, Prakash Ranjalkar.
*******
Kampuni ya mawasiliano ya kimataifa yenye shughuli katika nchi 20 mbalimbali Asia na Afrika, leo imeshiriki kuandaa semina ya GSMA inayofanyika Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo tarehe 12 na 13 Agosti 2014 katika hoteli ya Serena.
Semina hiyo ya kimataifa ya GSMA inalenga
zaidi kutazama maendelea ya sekta ya Mawasiliano kwa kuangalia Zaidi
mipango, mafanikio na fursa ya baadaye ya mawasiliano ya nishati mbadala
rafiki kwa mazingirana yaani –green telecoms, pia itaendesha
majadiliano juu ya mikakati inayowezekana kuongeza maendeleo katika
sekta ya mawasiliano kwa kuzingatia matumizi ya nishati rafiki kwa
mazingira (green power energy).
Semina
hiyo inahudhuriwa na makampuni kutoka mataifa yapatayo 60 ikiwemo
Tanzania, ambapo wanajadiliana na kubadilishana mawazo katika sekta ya
mawasiano.
Sunil
Colaso, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel alisema, “tunajisikia fahari sana
kushiriki katika mabadiliko ya nishati ya kijani yenye lengo la kutunza
mazingira ambayo yataleta faida kubwa katika jamii yetu. Ushirikiano
wetu na GSMA katika kuandaa tukio hili kutatuwezesha pia kuanzisha na
kuleta technolojia mpya ambapo tutachangia kwa kutoa mawazo yetu katika
mijadala inayohusiana na mawasilano endelevu nchini Tanzania na Afrika
kwa ujumla sehemu yetu ya kwa jamii (CSR)”.
“Mjadala
iliyoandaliwa itajikita zaidi katika mambo yanayohusu teknolojia na
maendeleo yake kama vile ufahamu kwenye teknolojia ya nishati ya jua,
yaani (solar hybrid technologies) au fuel cell technology na nyingine
nyingi. Baadaye, wasemaji mbalimbali wataangazia fursa za uwekezaji na
miundombinu ya biashara ambazo zitaweza kunufaika na uvumbuzi huu wa
matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala–rafiki wa mazingira kutumika
kwa maendeleo ya nchi ya Tanzania”.aliongeza Colaso
Akiongea
katika ufunguzi rasmi wa shughuli hiyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa aliwapongeza GSMA na Airtel kwa kazi
yao nzuri katika juhudi za kuleta maendeleo kwa jamii kwa kupitia
teknolojia ya mawasiliano. vile vile alishukuru sana GSMA
kuipa nafasi nchi ya Tanzania kuwa muandaaji wa semina hiyo muhimu kwa
mwaka huu. Pia kwa kutambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya
mawasiliano hasa kwenye swala la nishati ya kuwezesha minara nchini
Tanzania, Prof. Mbarawa alifurahishwa sana na mtazamo wa fulsa hiyo ya
utumiaji wa teknolojia ya nishati mbadala rafiki wa mazingira.
“kunachangamoto
kubwa katika Kuanzisha na kuendeleza miundombinu kwa kizazi kipya hasa
kwa nchi zetu zinazoendelea. Hivyo, tuna kila sababu ya kukaa na
kushirikiana jinsi ya kutumia teknolojia mbadala ili kwa pamoja
kupunguza changamoto za ukosefu wa nishati, na kuendeleza ufanisi wa
huduma na uhifadhi wa mazingira utakaofaidisha Afrika katika miaka
ijayo” , aliongea Mheshimiwa Mbarawa.
0 comments:
Post a Comment