Flaviana Matata ameongozana na Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin pamoja na wafanyakazi wa PSPF katika zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.
Mwanamitondo afanyae kazi zake za mitindo
nchini Marekani Flaviana Matata, yuko nchini kwa ajili ya kufanya kazi
za kijamii kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation. katika
mradi wa Back to school project /FMFstationarykit ambao unafadhiliwa na
mfuko wa penseni PSPF,
Baada ya mwezi
January Flaviana kugawa vifaa shule za msingi za jijini awamu hii
ameenda Mtwara na kufanikiwa kugawa shule za Msingi Mtua na Chemchem
ziliyopo Nachingwea pamoja nashule za msingi Litingi na Mnengulo
ziliyopo Lindi.
bado wanaendelea
kugawa vifaa hivyo kwa shule za msingi mikoa mingine "hadi sasa
tumeshagawa vifaa kwa watoto 700 na bado kuna kits 800 vitasambazwa
Tunduma ,Tunduru na Monduli"
Flaviana
alitoa shukran kwa PSPF kwa kudhamini huu mradi na akasisitiza makampuni
na mashirika kujaribu kuwezesha elimu kama hali halisi inavyoonekana
kwenye picha hadi leo kuna wanafunzi wanasoma chini na mti, na walio
madarasani,madarasa ni mabovu na hayana madawati.
0 comments:
Post a Comment