Mnamo tarehe 11/08/2014 majira ya 20:00 tulipokea taarifa
kutoka katika kijiji cha Bubutole Mbuyuni Kata na Tarafa ya Farkwa Wilaya ya
Chemba Mkoa wa Dodoma kuwa kuna mapigano ya wanakijiji, na mtu mmoja ameuawa na
wengine kujeruhiwa.
Mapigano hayo yalikuwa baina ya wanakijiji wa asili wa eneo
hilo na wasukuma ambao wamechukuliwa kama wageni jambo ambalo ni kinyume na
sheia za nchi.
Aliyeuawa katika mapigano hayo kwa kuchomwa mkuki kifuani
upande wa kulia ni DOGANI S/O LUPONDIJE mwenye miaka 48, Msukuma na Mkazi wa
Bubutole Wilayani humo.
Watuwengine saba (7) wamejeruhiwa na wanapatiwa matibabu
katika Zahanati ya Kwamtoro.
Jeshi la Polisi Mkao wa Dodoma linamsaka ADAMU S/O SWALEHE
Msandawe na ALLY S/O RAMADHANI ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Bubutole na
Mkoani Arusha kwani ushahidi unaonyesha ndio waliokuwa wanachochea vurugu hizo
zilizopelekea mauaji.
Chanzo cha mapigano hayo ni kile kinachodaiwa kuwa kunamradi
wa upimaji ardhi katika kijiji hicho unaoendelea kwaajili ya kuhamisha watu ili
lijengwe bwawa. Hivyo wenyeji wanadai itakuwaje walipwe fidia wageni ambao ni
wasukuma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma ametoa wito kwa wananchi
kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi na watambue kila raia ana haki ya
kuishi popote ilimradi havunji sheria za nchi.
Imetolewa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma
0 comments:
Post a Comment