Meneja msaidizi wa bia ya castle lite Victoria kimaro
kushoto akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam wakati
wakiwatangaza washindi sita wa kwanza wa shindano la Castle lite Yachy Party
ambapo washindi hao kila mmoja amejipatia kiasi cha shilingi laki moj.
**********
Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa
na Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) leo imetangaza washindi
wa wiki ya kwanza ya promosheni yake mpya inakayojulikana kama “Lite Up The Weekend”. Promotion hii ya
aina yake hapa nchini iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwezi Agosti, na itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu hadi mwezi Octoba
2014.
Akizungumza katika uzinduzi huo, meneja wa Bia ya Castle
Lite Geoffrey Makau alisema; Bia ya Castle Lite kama ilivyowatangazia
Watanzania hapo awali juu ya promosheni
hii kubwa na ya aina yake nchini na leo wameanza kuwapata washindi wao wa
kwanza ambao wameweza kujishindia kitita cha shilingi laki moja kwa kila mmoja
(100,000). Jumla wamepatikana washindi 6 katika wiki hii ya kwanza.
Hii ni promosheni kubwa inayoendeshwa nchi nzima. Na washindi
wetu wa leo walishiriki kwenye hii promosheni kupitia chupa za bia ambapo waliweza
kutuma nambari ya siri iliyopo chini ya kizibo cha bia ya Castle Lite.
Tunawajulisha
wateja wetu wapendwa wa castle lite kuwa tumewaandalia zawadi mbalimbali
zitakazokuwa zikitolewa kila wiki, ikiwa ni pamoja na zawadi za pesa taslimu
kama ambavyo tunawaona washindi wetu wa leo wakijishindia kitita cha fedha
taslimu.
Pamoja na pesa taslimu vili vile kuna zawadi nyingine kem
kem za kushindaniwa kama; zawadi za vifaa vya kusikilizia muziki (headfone),
tshirts, kofia pamoja na tiketi za
kuhudhuria matamasha mbalimbali yaliyodhaminiwa na Castle lite lakini zawadi
kubwa zaidi ni ile ya washindi kupata fursa ya kusherehekea kwenye VIP Party ndani
ya Boti la kifahari. Sherehe hii itajulikana kama “Castle Lite VIP Yacht Party”
Napenda kuwakumbusha wateja kuwa namna ya kushiriki
katika shindano hili ni kununua bia ya Castle Lite ya chupa yenye ujazo wa
mililita 375 au 330 na kuangalia chini ya kizibo cha Bia, ambapo utakuta namba
za siri, kisha utatuma namba hizo kwenda 15499 au kutembelea tovuti yetu ambayo
ni, www.castlelite.co.tz, ili upate nafasi ya kushinda zawadi za kila wiki au
zawadi kubwa ya “Castle Lite VIP Yacht Party”.
Kwa upande wake muwakilishikutoka Castle lite Victoria
Kimaro alisema kwa kipindi hiki cha promosheni, bia hiyo pia imeelezea jinsi ya kushiriki kwenye
promosheni hii kupitia ujumbe maalumu uliopo kwenye lebo ya nyuma ya chupa ya
Castle Liteili kuweza kumpatia mteja na mshiriki wa shindano hili urahisi wa
kutambua namna ya kupata maelekezo ya kushiriki.
Victoria alisema mabadiliko haya ya nembo hiyo ni
kwaajili ya kipindi cha miezi mitatu tu ambapo yatafikia ukomo pale shindano
litakapo malizika rasmi. Promosheni hii pia itapewa msukumo mkubwa kupitia
Radio, ambapo wapenzi wa Castle Lite watapigiwa simu na watatakiwa wapokee kwa
kuanza na neno ya “Lite Up My Weekend”. wateja watakaofanya vizuri watapata
zawadi mbalimbali kila wiki. Alisema Makau.
0 comments:
Post a Comment