wasanii wa bendi ya fm Academia wakiwa jukwaani wanaimba wapili kulia ni Rais wa bendi Nyoshi
Rapa wa bendi ya Fm Academia akiwa anashambulia jukwaa wakati wa shoo
Wanenguaji wa bendi ya Fm wakiwa kazini wote hawa watakuwepo katika uzinduzi huu wa Albamu ya Chuki ya nini usikose ni balaa.
*******
Fm Academia baada ya kukaa kwa muda wa miaka 4 (minne) yaani kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 sasa wanatarajia kuzindua rasmi album mpya kabisa inayojulikana kwa jina la Chuki ya nini ndani ya jiji la Arusha na vitongoji vyake .
Album ya chuki ya nini imebeba nyimbo kumi ndani yake,nazo ni:-Chuki ya nini, Fataki ,Otilia ,Ndoa ya kisasa,Neema,Dai chako ulaumiwe,Maisha,Madudu,Miraessa.album ya chuki ya nini ni album yenye kiwango cha kimataifa ambapo nyimbo hizi zote zitazinduliwa rasmi septembar tano mwaka huu ndani ya viwanja vya ukumbi wa Triple A jijini Arusha
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mkurugenzi wa SB Intamenti Seif Manyota alisema kuwa bendi hiyo inatarajia kutua jijini Arusha kwa kishindo kwa ajili ya uzinduzi huu wa albamu mpya ambapo alibainisha kua tukio hilo litakuwa la kihistoria.
Alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii kuzindua albamu nje ya mkoa wa dar es salaam na kwa hivyo wameamua kuwapa heshima kubwa wapenzi wa bendi hiyo wa mkoa wa Arusha pamoja na mikoa ya kanda ya kaskazini kwa ujumla hii ikiwa ni heshima ya kipekee.
"uzinduzi huu wa albamu sio tu tunazindua nyimbo mpya bali tunazindua pia vyombo vipya na staili mpya za kuicheza gwasuma kama vile mnavyojua bendi ya fm ni wazee wa pamba wazee wa kushambulia jukwaa"alisema Manyota
Aidha alibainisha kuwa kwa mkoa wa Arusha wameamua kuwapa kipaumbele na pia kwakuwa kunawapenzi wengi wa ngwasuma wameamua kufanya shoo hii nje ambapo ,kutafugwa jukwaa la kisasa kabisa.
Alitaja baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albamu ambayo inazinduliwa kuwa ni pamoja na Chuki ya nini,ndoa ya kisasa fataki pamoja na nyinginezo.
Aidha kwa upande mungine alisema uzinduzi huu autaishia Arusha tu bali wakazi wa Moshi na Tanga nao watapata burudani hii na kuzitambua staili mpya pamoja na nyimbo mpya zilizopo kwenye albamu hii.
Alisema kua pia kutakuwa na CD na DVD za albamu hiyo mpya iliyozinduliwa huku akisema kuwa kwa upande wa Arusha kiingili akuwa 20000 na unapatiwa CD moja buru mlangoni.
kwa upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi alisema kuwa timu yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa Arusha na kuwapa staili mpya ikiwemo ile ya vundesa ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha zaidi na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu pamoja na maneno matamu.
Alisema kuwa lengola kubwa la kuzindua albaimu hii apa jijini Arusha ni pamoja na kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo mpya na kuakikisha wapenzi wao wanajua staili zao zote za nyimbo hizo na sio ivyo tu pia alisema kuwa kwa kipindi hiki wanataka kuwa wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema wapo 32 na wote watafika jijini Arusha
0 comments:
Post a Comment