Nafasi Ya Matangazo

July 02, 2014

 Mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akimsikiliza kwa makini mwakilishi wa meneja wa TANESCO mkoa wa Iringa ambae  pia ni mhadisi wa mipango mkoa wa Iringa Bw Christopher Nguma wakati akieleza kuanza kwa mradi  huo jumatatu
 Viongozi wa serikali ya  kijiji cha Nindi  kata ya Lupingu wakifurahia ujio wa umeme katani kwao Lupingu
Mbunge  wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe  akisisitiza jambo  wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Lupingu juu ya kuanza kwa mradi wa umeme kata ya Lupingu ,huku  viongozi hao wakiwa  wamenyosha vidole  juu kuukubali mradi  huo.
**********

  
 MBUGE  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ageuka mbogo kwa wale  wenye nia ya kukwamisha maendeleo  jimboni awahakikishia   wananchi wa  kata ya Lupingu  kupata  umeme  kabla ya Krismass na  kuwa  zoezi la  kuanza kuchimba mashimo ya  kuweka nguzo  za umeme  litaanza  jumatatu likiongozwa nay eye  mwenyewe .

Huku akiwapata  wananchi  wa kata ya  Lupingu  kutomchagua  diwani  wao katika uchaguzi mkuu  wa mwaka 2015  iwapo atashindwa  kushiriki  kikamilifu katika usimamizi na ushiriki wa  maendeleo katika mradi  huo.

Mbunge Filikunjombe  alitoa ahadi  hiyo iliyopokelewa kwa  shangwe  kubwa na wananchi wa  vijiji  vitatu  vya kata ya Lupingu  leo  wakati alipoongozana na wataalam wa shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) katika vikao vya pamoja na viongozi wa  serikali  za mitaa na uongozi wa  wilaya na ule  wa Tanesco mkoa  na  wilaya ya  Ludewa .
 
Alisema  kuwa amelazimika  kupigania umeme  katika vijiji  mbali mbali vya  jimbo la Ludewa kama  sehemu ya kuwakumbuka wananchi  wake na  kuongeza idadi ya  vijiji vya  jimbo hilo la Ludewa kuwa na umeme  kutoka  kijiji kimoja alichokikuta wakati akiingia madarakani hadi  vijijini zaidi ya 10 sasa ambavyo   vina uhakika  wa kupata  umeme na baadhi tayari  vimepata  umeme  tayari .

Hivyo alisema  itapendeza  kuona wananchi na vijiji  vyote  vya kata ya Lupingu ambavyo ni pamoja na Nindi ,Ntumbati na Lupingu kupata  umemne kabla ya sikukuu ya krismasi na kuwa akiwa kama mbunge hatapenda kuona mtu ama kiongozi  yeyeyo anakwamisha mradi  huo kwa  wananchi .

“Napenda  kuwa mkweli katika  hili lengo la serikali ya  chama cha mapinduzi  ni kuona  wananchi  wake  wanaendelea  kupata maisha  bora  na  si kwa  wana CCM pekee ni  wote hata  wapinzani kwani maendeleo ya umeme na mengine  hayajawalenga  wana CCM ni wote  …..sasa  kama  hivyo  ndivyo ni lazima  wananchi  wote  kushiriki maendeleo  yetu na Yule atakayekwamisha  tutashughulika nae na katika  hili nitakuwa mkali  zaidi” alisema mbunge  Filikunjombe 

Kuwa iwapo  mtendaji wa  serikali ya kijiji  mwenyekiti au  diwani watabainika  kuwa  ni kikwazo katika uendelezaji wa maradi  huo basi  ni wazi watawajibishwa  wao kwanza ili  kuonyesha mfano wa  wananchi  kushiriki kupokea miradi.

Mbunge  huyo alisema kuwa kama mbunge atakuwa msitali wa mbele  kuunga mkono maendeleo  hayo na katika  kuwaonyesha mfano  wananchi hao kuwa  hawakukosea katika kuchagua  siku ya jumatatu atafika  eneo la mradi  mapema asubuhi akiwa na vitendea kazi kwa ajili ya kuungana na  wananchi wa kata ya Lupingu katika uchimbaji wa mashimo ya nguzo za umeme  .

Katika hatua  nyingine  mbunge  Filikunjombe aliipongeza  wizara ya ujenzi kwa  kuwaondolea kero ya  miundo mbinu wakazi wa kata hiyo ya Lupingu ambao siku  zote  walikuwa  wakitembea  zaidi ya kilometa  zaidi ya 30 kwa miguu  kuelekea  mjini Ludewa kupata huduma mbali mbali kutokana na ubovu wa barabara ila kwa sasa wananchi hao  wamepatiwa barabara ya uhakika na tayari kuna usafiri wa daladala unaotoa huduma maeneo hayo kila  siku.
Posted by MROKI On Wednesday, July 02, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo