Na Andrew Chale, Bagamoyo
CHUO cha Kilimo na
Mifugo Kaole (Kaole College of agriculture (KCA), kesho Jumamosi Julai 12,
kinatarajia kufanya mahafali yake ya pili chuoni hapo huku wahitimu 291, wakitarajiwa kutunukiwa vyeti
mbalimbali.
Akizungumza mjini hapa,
principle wa chuo hicho, Cuthbert
Liwa alisema kuwa, tayari maandalizi yamekamilika na mahafali hayo yatafanyika
kwenye viwanja vya chuo hiko.
“Jumla ya wahitimu 291, wanatarajiwa kuhitimu na
kutunukiwa vyeti vyao. Kati ya hao, wahitimu 179, fani ya Kilimo
na wahitimu 112, kwa fani ya Ufugaji”
alisema Liwa.
Aidha, alisema mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, anatarajiwa
kuwa Dr. Masuruli wa Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi.
Aidha, aliwaomba watu mbalimbali kujumuika kwa pamoja kwenye
mahafali hayo, chuoni hapo, Kaole, Bagamoyo. (the college is located in
South-East Bagamoyo 3.5 km from Bagamoyo township in the premises of Kaole
Secondary school. The centre is along
the showers of the Indian Ocean).
0 comments:
Post a Comment