Nafasi Ya Matangazo

July 08, 2014

Mbunge wa Viti Maalum (UVCCM)  mkoa wa Arusha Catherine Magige akiwajulia hali baadhi ya majeruhi nane wa mlipuko wa bomu uliotokea usiku wa kuamkia jana katika mgahawa wa Vama Traditinal Indian Culture jijini Arusha.
 Miongoni mwa majeruhi hao wapo wanne wa familia moja ambao ni baba mama na watoto wao wawili ambao walijeruhiwa na bomu hilo huklu mmoja akikatwa mguu.
Majeruhi ambaye alikatwa mguu kushoto kutokana na mlipuko huo.  
*******
Mbunge wa viti Maalum kupitia chama cha mapinduzi CCM Mh.Catherine Magige amelaani vikali  tukio la Bomu lililotokea katika mgahawa wa VAMA Tradition Indian Culture  jijini Arusha huku akiitaka serikali kuwachukulia hatua kali kwa wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo

Mh.Magige aliyasema hayo leo katika hospitali ya Selian wakati alipowatembelea majeruhi nane Raia wa Asia waliolazwa katika hospitali hiyo ambapo wengi wa majeruhi waliumia katika maeneo ya miguu,mikono na tumboni hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi kupoteza mguu wake wa kushoto

Magige alisema kuwa kutokana na matukio ya aina hiyo kutokea kwa mfululizo, hali hiyo imesababisha jiji la Arusha kupoteza amani ili hali Tanzania ni Nchi ya Amani'

"Inasikitisha sana kwa kweli matukio kama haya kujirudia rudia inatia hofu sana kwa wakazi wa Arusha pamoa na wageni wanaokuja katika jiji letu"alisema

Aidha alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa vyombo vya dola kufanikisha kukamatwa kwa wale wote wanaohusika na matukio ya uvunjifu wa amani.
Posted by MROKI On Tuesday, July 08, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo