WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKATI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV MARA
KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA
IRAMBA BUNDA NA MAJITA MUSOMA VIJIJINI. KUTOKA KUSHOTO NI KAIMU MKUU WA MKOA WA
MARA MHANDISI EVARIST NDIKILO AKIFATIWA NA MBUNGE WA JIMBO LA MWIBARA ALPHAXAD
KANGI LUGORA, WENGINE KUTOKA KULIA NI KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI MHANDISHI
MUSSA IYOMBE AKIFATIWA NA MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO PAMOJA NA
MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA.
KIVUKO KIPYA CHA MV MARA KAMA KINAVYOONEKANA
KATIKA PICHA KABLA YA KUFUNGULIWA
*********
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John P. Magufuli amewataka
wakazi wa Iramba na Majita kutunza kivuko kipya cha MV Mara ili kiweze
kuwasaidia katika kuinua uchumi wa maeneo hayo.
Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana kabla ya kuzindua
kivuko hicho kipya katika kijiji cha Iramba wilayani Bunda mkoani Mara.
“Ndugu zangu wa Iramba kitunzeni kivuko hiki
kwani ni mkombozi mkubwa katika kuwaletea
maendeleo yenu pamoja na maeneo ya
jirani” Alisema Waziri Magufuli.
Pia Waziri Magufuli aliwaasa wavuvi kutotega
nyavu kwenye njia za kivuko ili kiweze kudumu kwa muda mrefu kwani kwa kufanya
hivyo watasababisha injini za kivuko hicho kuharibika mapema.
Aidha Waziri Magufuli aliwapongeza Mbunge wa
Mwibara Kangi Lugora pamoja na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kwa juhudi
zao zilizochochea kupatikana kwa kivuko hicho.
Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 25,
yaani magari manne 4 na abiria 50, kitaokoa maisha ya wananchi wengi ambao
walikuwa wanapata adha kubwa ya usafiri kutokana
na kukosa usafiri wa uhakika ambao ulikuwa unahatarisha maisha yao.
“Nimeambiwa hapa nauli ilikuwa Shilingi 2000/=
kuvuka upande wa pili kwa kutumia boti za watu binafsi lakini kwa kivuko hiki
natangaza rasmi kuwa nauli kwa kivuko
chetu kipya ni shilingi 500/= tu, na wanafunzi waliovaa sare watapanda bure,
watoto sh.100” Alisema Waziri Magufuli
Dkt.Magufuli aliongeza kuwa nauli za magari na
mizigo zitapangwa na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ambao ndio wasimamizi wa kivuko
hicho.
Aidha, Waziri Magufuli aliongeza kuwa Serikali
itaendelea kuboresha miundombinu bila kuangalia itikadi zozote za kisiasa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya
wakazi wa kijiji cha Iramba, walisema kuwa walikuwa wanapata taabu sana ya usafiri
kwani ilikuwa inawalazimu kuvuka kwa mitumbwi ambayo ilikuwa inahatarisha
maisha ya wakazi wa maeneo hayo.
0 comments:
Post a Comment