Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Dk.Binilith Mahenge akizindua rasmi tovuti ya mabadiliko ya tabianchi
itakayotumika kutoa taarifa mbalimbali za utunzaji wa Mazingira.Kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Julius Ningu.
******
SERIKALI kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, leo imezindua tovuti ya mabadiliko ya tabia nchi.
Akizindua tovuti hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Dk.Binilith Mahenge amesema mbali na mambo mengine lakini itakuwa ikitoa habari mbalimbali za masuala ya madiliko ya tabia nchi lakini pia itakuwa ikitoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabia nchi.
Katika hotuba yake fupi ya uzinduzi wa tovuti hiyo,
aliyoandaliwa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark, Mhenge amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya
nchi huangaliwa kwa muda wa miaka 30 hivyo kwa kipindi hiki chote kumekuwa na
madhara mengi yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia Nchi ikiwa ongezeko
la joto, kina cha bahari kuongezeka pamoja na ongezeko la majanga ya mvua
zisizo na viwango, kutoka na shughuli za
binadamu katika uzalishaji hasa viwanda vikubwa
Alisema kwa tovuti inayozinduliwa ina umuhimu mkubwa kwani
inaelezea maeneo ya hali ya mabadiliko ya tabia
nchi na juhudi za serikali katika kukabiliana na athari zinazoletwa na
mabadiliko hayo.
“ziko sababu za kuungana na wenzetu ili kuondoa tatizo hili la mabadiliko ya nchi ambapo
tovuti hii www.climatechange.go.tz
inatuunganisha na tovuti mbali mbali katika kupunguza gesi joto hapanchini pia
inaelezea fursa zilizopo katika miradi na program mbali mbali. Alisisitiza”
Alibaini kuwa tovuti hii itachangia kwa kiasi kikubwa
kuongeza uelewa na weledi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi nchini kwa wananchi na wadau kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment