Nafasi Ya Matangazo

June 18, 2014

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo akiwaongoza washindi wa tiketi ya Winda SAFARI YA Brazil na Serengeti mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere. Nyuma ni Bi Juliana Joseph Masawe(mshindi)
Menrad Faustin Shayo kutoka Arusha akihojiwa na waandishi mara baada ya kurejea nchini. Bw. Shayo alielekea nchini Brazil baada ya kushinda tiketi kupitia kampuni ya bia ya Serengeti. Shayo aliambatana na washindi wawili katika ziara ya utembelea vivutio mbalimbali.
Pilikapilika za washindi mara baada ya kuwasili nchini kutokea Brazil kula bata baada ya ushindi kupitia kampeni ya Winda Tiketi ya Brazil na Serengeti iliyokuwa ikichezeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Lager. Kulia ni Deusdedit Kahwa kutoka Dar es Salaam, Bi Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro (katikati) pamoja na kushoto ni mwenyeji wa washindi hao Bw. Allan Chonjo Meneja Masoko wa kampuni ya Serengeti.
***********
Washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti waliokwea pipa wiki iliyopita kuelekea nchini Brazil kutembelea vivutio mbalimbali wamerejea kwa shangwe kubwa baada ya kuyaona maisha mapya ya bara jingine. Ziara yao ilichukua siku tano nchini Brazil huku washindi hao wakila bata katika vivutio mbalimbali nchini Brazil.

Washindi wa tiketi hizo Bi Juliana Joseph Masawe kutoka Kilimanjaro, Deusdedit Kahwa kutoka Dar es Salaam pamoja na Menrad Faustin Shayo kutoka Arusha wamerejea nchini wakiwa na mwenyeji wao Bw Allan Chonjo ambaye ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti. Washindi hao walijishindia tiketi hizo baada ya kutumia bia ya Serengeti na kufungua chini ya kizibo ili kushinda na hivyo walijipatia tiketi za kwenda nchini Brazil kutembelea vivutio mbalimbali.

Juliana Joseph Masawe amewapongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwa wakweli na kuwajali wateja wao. “Sitasahau starehe nilizoziona nchini Brazil. Siku tano zimakuwa kama siku mbili. Nilitamani kukaa mwezi. Najivunia kutumia bia ya Serengeti kwani imenionjesha maisha tofauti kabisa. Mwanzo nilijihisi uoga kwani sikuwahi kupanda ndege lakini kupitia bia ya Serengeti nimepanda ndege, nimetembelea vivutio mbalimbali, nimeona makanisa makubwa mno sijawahi kuona, mashamba makubwa ya mpunga na mihogo pia nimekutana na watu wapya kabisa katika maisha yangu”.  

Nae Menrad Faustin Shayo kutoka Arusha  alishindwa kujizuia kwa furaha wakati akihojiwa katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere “Sio siri najiona mpya kabisa sikutegemea kufika nchini Brazil katika maisha yangu, kila promosheni itakayotolewa na Kampuni ya bia ya Serengeti  lazima nitashiriki kwa sababu hawana upendeleo kabisa kama ni mshindi basi utapewa kile unachostahili. Kampuni ya bia ya Serengeti imenifanya niwe na kitu cha kuhadidhia maisha yangu yote, naamini familia yangu itafurahi zaidi nikiwapa habari za nchini Brazil.

Mwenyeji wa washindi hao Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti  Bw. Allan Chonjo amewashukuru sana washinidi kwa kuichagua bia ya Seregeti na kushiriki katika promosheni ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti. “Ninaamini mmefurahia ushindi wenu. Bila shaka mtakuwa mabalozi wa bia ya Serengeti kila mtakapokuwa. Promosheni hii ililenga kawashukuru wateja wetu kwa kuichagua bia ya Serengeti kuwa kinywaji chao. Tumerudisha fadhida kwa wateja wetu kama shukrani kwao kwani bila wao sisi tusingeweza kusonga mbele”.
Posted by MROKI On Wednesday, June 18, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo