Mwendesha pikipiki na abiria (majina hayakutambulika kwani walikuwa
hawawezi hata kuongea) wakiwa wamelala chini katika barabara ya Chalinze
Segera karibu na Kabuku baada ya kugongwa na gari dogo lenye namba za usajili T818 BNS leo mchana.
Bodaboda hiyo ilikuwa imepakia abiria wawili kwa staili ya mshikaki ambayo ni kinyume cha sheria za usalama barabarani huku kofia ngumu ikiwa ilivaliwa na dereva na ilimvuka baada ya ajali hiyo.
Mpiga picha wa tukio hili ambaye ni mdau wa blog hii, Rodney Thadeus, alienda kutoa
taarifa ya ajali kiyo cha polisi cha Kabuku ambapo Polisi walienda
kutoa msaada wa kukimbiza majeruhi hospitali pamoja na kupima ajali.




0 comments:
Post a Comment