Nafasi Ya Matangazo

May 01, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa serikali na wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)  wakiangalia maandamano ya wafanyakazi wakati wanaingia uwanjani hapo leo katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Naibu Rais TUCTA, Notburga Masikini na Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicolaus Mgaya na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 Mdundiko ulioendelea
 Benki ya Twiga Bancorp ilishiriki maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya wafanyakazi kwa chini ya Chama chao cha Wafanyakazi TUICO na kujumuika na wafanyakazi webnzao duniani kopte katika maandamano kama inavyoonekana pichani.
 Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania wakishiriki katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Kitaifa Jijini Dar es Salaam leo.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN, nao walishiriki katika maandamano hayo.
Wafanyakazi wa Uhuru FM nbao walishiriki Kikamilifu katika maandamano ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
 
 Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu-Tanzania (NIMR) nao walikuwepo na waliwakilishwa na  NIMR Muhimbili na waliongozwa na kauli mbiu yao ya 'Utafiti kwa Afya Bora Na Ustawi wa Jamii'.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Steve Gannon akionesha sha furaha kwa siku ya wafanyakazi
 
 Kampuni ya Bia ya Serengeti nayo ilishiriki katika maadhimisho hayo na pichani ni wafanyakazi wake wakiwa uwanjani hapo.

Benki ya Posta Tanzania (TPB) ni moja ya taasisi za fedha zilizo shiriki maadhimisho hayo. 
 Askari wa Wanyama Pori wakishiriki katika maadhimisho hayo na katika gari ni ngozi ya Mamba

Posted by MROKI On Thursday, May 01, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo