Washiriki wa Miss Tabata 2014
wakiwa mazoezini Da’ West Tabata.
******
Na Mwandishi Wetu
Bendi ya African Stars “Twanga
Pepeta” itasindikiza uzinduzi wa Redds Miss Tabata itakayofanyika Jumapili ya
Pasaka katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph
Kapinga amesema bendi hiyo itatambulisha nyimbo zao mpya kama zawadi yao ya Pasaka
kwa wapenzi wao.
Pia bendi hiyo ijulikanayo
kama Wakali wa Kisigino pia watapiga nyimbo zao zote kali hadi majogoo.
Mratibu huyo wa Bob
Entertainment na Keen Arts alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya
kuwaona warembo hao siku hiyo kabla hawajashiriki kwenye shindano la Miss
Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.
Katika uzinduzi huo warembo wa
Tabata watasindikizwa na washiriki wenzao wa Miss Mzizima na Miss Ukonga.
Pia watakuwepo viongozi
waandamizi kutoka kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga na
Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa.
Warembo 21 wanaendelea na
mazoezi ya Miss Tabata katika ukumbi wa Da West Park chini ya wakufunzi wawili
- Neema Chaki na Pasilida Bandari.
Warembo hao ni Esther Frank
Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias
Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18), Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20),
Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wenine ni Annatolia Raphael
(21), Mary Henry (21), Evodia Peter
(22), Fatma Hussein Ismail (20), Ester
Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi (21), Najma Charles
Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19) na Ramta Mkadara (20).
Warembo watano kutoka Tabata
watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.Mrembo anayeshikilia taji la
Miss Tabata ni Dorice Mollel ambaye pia ni
Redds Miss Ilala.
0 comments:
Post a Comment