Watoa huduma
wa shirika linalo jishungulisha na masuala ya afya la PSI Tanzania
wakiendesha zoezi la upimaji wa Saratani ya shingo ya kizazi katika
jukwaa la FAMILIA KITCHEN PART GALA 2014 iliyofanyika katika ukumbi wa
Kilimani mjini Dodoma.
Baadhi ya
wanawake wakijisajiri tayali kabra ya kuingia katika jukwaa la FAMILIA
KITCHEN PART GALA 2014 ambapo zaidi ya wanawake 300 walijumuika katika
jukwaa na kuhamasika kushiriki katika zoezi la upimaji afya zao ikiwemo
ukimwi na saratani ya shingo ya kizazi.
Mwanamuziki
maarufu hapa nchini Shilole akitumbuiza wanawake katika onesho maalum
alilo lifanya katika FAMILIA KITCHEN PART GALA 2014 ambapo zaidi ya
wanawake 300 walijumuika katika jukwaa na kuhamasika kushiriki katika
zoezi la upimaji afya zao ikiwemo ukimwi na saratani ya shingo ya
kizazi.
Mwanamuziki
maarufu hapa nchini Shilole akitumbuiza wanawake katika onesho maalum
alilo lifanya katika FAMILIA KITCHEN PART GALA 2014 ambapo zaidi ya
wanawake 300 walijumuika katika jukwaa na kuhamasika kushiriki katika
zoezi la upimaji afya zao ikiwemo ukimwi na saratani ya shingo ya
kizazi.
Mwazirishi wa
jukwaa la FAMILIA KITCHEN PARTY GALA 2014 bi Vida Mndolwa (katikati)
akizungumza jambo na wanawake waliohudhulia jukwaa hilo hawapo pichani
(kushoto) ni meneja wa uzazi wa mpango shirika la PSI Tanzania bi
Catherine Paul (kulia) aliye kuwa mshehereshaji katika jukwaa hilo.
Baadhi ya
wanawake waliojitokeza kwa wingi katika jukwaa la FAMILIA KITCHEN PARTY
ambalo limefanyika mjini Dodama katika ukumbi wa kilimani, wanawake
zaidi ya 300 walijumuika katika jukwaa na kuhamasika kushiriki katika
zoezi la upimaji afya zao ikiwemo ukimwi na saratani ya shingo ya
kizazi.
WANAWAKE zaidi ya 300
wamejitokeza kupewa semina ya uzazi wa mpango, saratani ya shingo ya
kizazi na elimu kuhusu ugonjwa wa Ukimwi iliyoandaliwa na Shirika
linalotoa Elimu ya Afya la PSI Tanzania mjini Dodoma.
Mbali ya kushiriki
katika semina hiyo, wanawake 90 walipima afya zao papo hapo baada ya
kupata elimu, huku waandaaji wakisema uelewa mdogo ni kiini kikubwa cha
wanawake kushindwa kupima afya zao ili kujitambua.
Akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa semina hiyo, Meneja wa Huduma ya Uzazi wa Mpango wa
PSI, Catherine Paul alisema bado uelewa kuhusu uzazi, saratani ya
shingo ya kizazi, Ukimwi, malezi ya watoto ni tatizo kwa wanawake wa
mijini na vijijini.
“Kwa kweli mwitikio
umekuwa mkubwa kuliko hata vile tulivyotarajia.Kama inavyofahamika
ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi hivi sasa ni tishio kubwa na
takwimu zinaeleza kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi
kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki,” alisema.
“Leo tunashuhudia na
kufurahi kuona kuwa wanawake hawa zaidi ya 300 wamekutana hapa ili
kubadilishana mawazo na kupata elimu kwa mambo yanayowahusu hatua
itakayosaidia kwa kiasi kikubwa kubadili mifumo yao ya maisha baada ya
kujitambua,” alisema.
Kwa upande mwingine,
Mratibu wa Mradi wa Afya ya Mama na Mtoto, Khadija Ameir alisema PSI
imekuwa inatoa elimu kuhusu masuala hayo katiika maeneo mbalimbali ya
mijini na vijijini kwa lengo la kumkomboa mwanamke na kustawisha maisha
yake.
Alisema katika maeneo ya
vijijini Shirika hilo limekuwa likiendesha kampeni ya nyumba kwa nyumba
ili kuwafiki wanawake na kuwapa elimu kuhusu uzazi wa mpango, saratani
ya shingo ya kizazi, Ukimwi na malezi ya Mama na Mtoto, hatua ambayo
imeongeza idadi ya wanawake ambao sasa wanatambua kuhusu afya ya uzazi.
“Ikumbuke kwamba PSI
inawatumia wataalamu katika kufikisha elimu hii kwa wanawake hatua
ambayo imesaidia kupunguza idadi ya vifo vya wanawake kutokana na
masuala ya uzazi, Ukimwi na hata saratani ya shingo ya kizazi, huku pia
vifo vya watoto chini ya miaka mitano vikipungua,” alisema Ameir.
Akizungumza, Mratibu wa
mafunzo hayo kutoka Asasi ya Women in Balance (Mizania ya Wanawake),
Vida Mndolwa alisema mwitikio wa wanawake katika kujitokeza kupata elimu
wa afya ya uzazi, Ukimwi na saratani ya shingo ya kizazi umekuwa mkubwa
kila mahala ambapo wanafika kutoa elimu hiyo.
“Kama mnavyoona hapa
Dodoma mwitikio umekuwa ni mkubwa sana na tunashukuru kuona wanawake
wamejitokeza ili kupata fursa ya kukutana na wataalamu wa huduma za afya
suala ambalo litaongeza uwezekano wa wao kujitambua na kuwa na maisha
yaliyo bora na salama,” alisema Mndolwa.
Mmoja wa washiriki
Mwanajuma Othman Mtuli alisema;” Ni zaidi ya elimu, ni zaidi ya
burudani, ni zaidi ya mafunzo. Kwa kweli semina hii imetusaidia kufahamu
kuhusu kujua umuhimu wa malezi ya watoto, kutunza ndoa na hata
ujasiriamali na hivyo tunaishukuru sana PSI kwa mafunzo haya.”
0 comments:
Post a Comment