Mbunge wa Viti Maalum kwa vijana kupitia Chama cha Mapinduzi
(CCM), Ester Bulaya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
mashindano ya Ester Cup yatakayofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba na uwanja wa
Shule ya Msingi Bunda. Na
********
Mwandishi Wetu
Jumla ya timu 72 zitashiriki katika
mashindano ya soka ya Ester Cup ambayo huandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, kwa tiketi ya vijana wa Chama
cha Mapinduzi (UVCCM), Ester Bulaya.
Mashindano hayo, yanafanyika mwaka huu
kwa msimu wa nne katika Jimbo la Bunda, na yatachukua nafasi katika viwanja vya
Sabasaba, Shule ya Msingi Bunda, Nyamswa na Mgeta.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
jana (leo), Bulaya alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa kulinganisha na miaka
ya nyuma.
Alisema kuwa mwaka 2011 jumla ya timu 18
zilishiriki, mwaka 2012 timu 26 wakati mwaka jana ziliongezeka mpaka 38.
Bulaya alisema, ameamua kuendeleza
mashindano hayo ili iwe fursa ya ajira kwa vijana wenye vipaji vya soka.
“Mimi ni mzaliwa wa Bunda na moja ya
changamoto za jimbo letu ni kutokuwa na mashindano ya soka, nilipoanzisha
mashindano ya Ester Cup nilileta kuhamasisha michezo jimboni kwetu, nafurahi kwa
sasa lengo limetimia na hamasa katika jimbo hilo imeongezeka,” alisema Bulaya.
Alisema, tangu kuanza kwa mashindano,
wilaya ya Jimbo la Bunda na wilaya nzima ya Bunda, imepata mafanikio makubwa na
wachezaji wengi wamepata ajira kwenye klabu mbalimbali kubwa zinazoshiriki
michuano mikubwa nchini.
Alifafanua kuwa ili kuleta maendeleo
katika michuano hiyo, wamezuia wachezaji nje ya jimbo la Bunda kucheza Ester
Cup jambo ambalo halitasaidia malengo yetu ya kuendeleza michezo kwa vijana wa
jimbo husika.
Bulaya alisema kuwa jumla ya Sh15.4
zimetumika kugharimia mashindano ya mwaka
ambapo mshindi atapata Sh 1.5 million ambapo mshindi wa pili atazawadiwa
Sh700,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa Sh 500,000.
Aliongeza kuwa pia amefanikiwa kugawa
vifaa mbali mbali kwa wilaya nne na kata 150 za wilaya nne, shule za sekondari na
kutumia jumla ya Sh 75 million. Alisema kuwa wilaya ya Rorya na Tarime pekee
ndizo hazijapata msaada huo na yupo mbioni kuwakabidhi.
0 comments:
Post a Comment