Na Mwandishi Wetu
MAZOEZI ya warembo watakaowania taji la
urembo la Sinza, Miss 2014 yataanza Mei 5 kwenye ukumbi wa Meeda uliopo Sinza
Mori na Lufungila jijini.
Taji la Miss Sinza linashikiliwa na Miss
Tanzania, Prisca Clement alimaliza katika hatua ya 10 bora katika mashindano ya
mwaka jana ya Miss Tanzania na pia alishinda taji la mrembo mwenye kipaji
katika mashindano hayo.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary
alisema kuwa maandalizi ya mazoezi hayo yamekamilika na yatasimiwa na kamati ya
maandalizi huku ikitafuta mwalimu kwa ajili ya kuwanoa.
Majuto alisema kuwa warembo waliowahi
kushiriki mashindano hayo wanaruhusiwa kuja kutoa sapoti kwa warembo wapya na
kamati yao itawapa nafasi ya kuwafundisha warembo wapya ili kuwapa ‘mbinu’
mbali mbali za mashindano hayo.
Alisema kuwa fomu za kuomba kushiriki
katika mashindano hayo zinapatikana kuanzia leo (Ijumaa) maduka ya Zizzou,
Sinza Afrika Sana, Meeda, Ofisi za Miss Tanzania na Ofisi za gazeti la
Mwananchi (Tabata reline.
“ Lengo letu kubwa ni kurudisha hadhi ya
Miss Sinza, Kinondoni katika mashindano ya mwaka huu, tumejipanga kulinda
heshima yetu na tunaamini titafanikiwa kwa heshima ya wakazi wa Sinza,
Kinondoni na Tanzania kwa ujumla,” alisema
Majuto.
Alisema kuwa wanawakaribisha warembo
wanaotaka ‘kupata taji’ kuchukua fomu zao ambazo zinatolewa bure. Majuto pia aliwaomba wadhamini wanaotaka
kujitangaza kupitia mashindano yao wanaruhusiwa kuja kudhamini mashindano hayo
na milango ipo wazi.
0 comments:
Post a Comment