Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na
Waziri wa Afrika Mashariki, Samweli Sitta leo amefanya ziara kwa
viongozi wakuu wa kidini kwa lengo kuwaambia kile kinachoendelea ndani
bunge hilo ambalo linaendelea na shughuli zake mjini Dodoma.
Akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali
vya habari katika ofisi za Makao Makuu ya Bakwata, Kinondoni jijini Dar
es Salaam, Sitta amesema amelazimika kufanya hivyo akiamini viongozi hao
wana kundi kubwa la watu nyuma yao hivyo ni vyema wakawa wanasisitiza
amani na umoja ndani ya taifa.
Mwenyekiti huyo alianzia makao makuu ya
Kanisa Katoliki na kuonana na Mhadhamu Kadinali Pengo na kuzungumza naye
faragha na baada ya hapo alimtembelea Shehe Mkuu wa Tanzania, Issa bin
Simba na kufanya naye mazungumzo ya faragha pia.
Baada ya hapo, kiongozi huyo aliongea na
waandishi wa habari na kusisitiza kuhusu kamati zilizoundwa kwa lengo la
kufanikisha mchakato mzima wa kupata katiba mpya.
Picha, habari: Haruni Sanchawa- GPL.
0 comments:
Post a Comment