Nafasi Ya Matangazo

April 07, 2014

MATOKEO RASMI JIMBO LA CHALINZE;-RIDHIWAN JAKAYA KIKWETE;-
Hatimaye Ridhiwani Kikwete aibuka kidedea ubunge Chalinze kwa 86.61% akiwa amepigiwa kura na wakazi 20,828.

matokeo yametangazwa sa 9 usiku wa leo.

Mathayo Torongei ameshika nafasi ya pili na alipata kura 2,544 sawa na 10.58%,huku Mgombea wa CUF Bw.Fbian Skauki akishika nafasi ya tatu akiwa na kura 476 sawa na 1.98%,Chama cha AFP kikishika nafasi ya nne kupitia mgombea wake Ramadhani Mgaya akiwa na kura 186 sawa na 0.59% na nafasi ya mwisho ni ya Hussein Ramadhani kupitia chama cha NRA aliyepata kura 60 sawa na 0.25% huku kura 375 zikiharibika.

Waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni wakazi elfu 92,waliopiga kura ni watu 24,422 idadi inayotajwa kushuka toka katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2010 ambapo wapiga kura katika jimbo hilo walikuwa zaidi ya elfu 36.
Posted by MROKI On Monday, April 07, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo