Timu ya Soka ya Tanzania, Tiafa Star imelazimishwa sare ya bao 1-1 na wenyeji Brave Warriors ya Namibia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa usiku huu uwanja wa Sam Nujoma, Katutura- Windhoek Namibia leo.
Goli la Stars lilifungwa kwa njia ya kona na mchezaji Mcha Hamisi Mcha kunako dakika ya 86 na wenyeji kusawazisha dakika tisa baade kupitia mcheszaji Nekundi Haleluya Panduleni. Hadi dakika ya 97 ya kipenga cha mwisho cha mwamuzi Tanzania 1 Namibia 1 matokeo ambayo yamemnusuru kocha Ricardo Manentti na benchi zima la ufundi la Brave Warriors ambao wamekuwa na matokeo mabaya kwa micxhezo zaidi ya minne ya kimataifa waliocheza.
Stars inayonolewa na makocha wa muda wazawa, Salum Madadi na Hafidhi Badru Iliwashusha dimbani Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Abdi Banda, Agrey Moris (C), Said Moradi, Hamid Mao Mkami, Ramadhani Singano, Amri Kiemba, Juma Luzio, Jonas Mkude, Harini Chanongo na benchi walikuwepo Shabani Kado, Michael Pius, Athanas Mdani na Mcha Hamis Mcha.
0 comments:
Post a Comment