Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2014

FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI –CUF
 
DHIDI YA

MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO -CHADEMA
13.03.2014
                                                                                                               
Mimi  FABIAN L. SKAUKI, mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la CHALINZE kwa Ticket ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo.
 
1.       Ndugu MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.
 
2.       Ndugu MATHAYO .M. TORONGEY amejaza  katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza, na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea.
 
3.       Ndugu MATHAYO .M.TORONGEY  amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea. Ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika. Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.
 
4.       Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la CHALINZE, na kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.
 
Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
Posted by MROKI On Thursday, March 13, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo