Mkurugenzi wa Mipango Mikakati wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB
Development Bank), Jaffar Machano akifungua mkutano huo wa hafla ya
utiaji saini mkataba wa makubaliano.
********
Nwa mwandishi wetu,
Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank) na Benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Development Bank of Southern Africa, DBSA) zimeingia mkataba wa makubaliano ya kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini jana jioni.
Makubaliano hayo yatasaidia kufufua miundombinu ya uchukuzi
ikiwemo Reli ya Kati, Viwanja vya Ndege vya Arusha na Mwanza pamoja na
Upanuzi wa Bandari.Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank) na Benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Development Bank of Southern Africa, DBSA) zimeingia mkataba wa makubaliano ya kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini jana jioni.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana jioni.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Peter Noni akizungumza na wadau wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (DBSA), Patrick Dlamini akizungumza na wadau katika hafla hiyo.
Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Kiserikali,Bunge na Binafsi wakifuatilia matukio ya hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick
Dlamini, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development
Bank), Peter Noni wakifuatilia kwa makini sehemu ya matukio wakati wa
hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank),
Peter Noni (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick
Dlamini (wa pili kushoto) wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya
ushirikiano wa kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi huku ukishuhudiwa na
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia waliosimama)
na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia waliosimama). Kushoto
(waliokaa) ni Meneja Mkuu wa Fedha wa DBSA, Bane Makene na Mwanasheria
wa Bodi ya TIB Development Bank, Martha Maeda (kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank),
Peter Noni (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick
Dlamini (wa pili kushoto) wakibadilishana nyaraka baada ya kutiliana
saini mkataba wa makubaliano ya
ushirikiano wa kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini. Kushoto ni
Meneja Mkuu wa Fedha wa DBSA, Bane Makene na Mwanasheria wa Bodi ya TIB
Development Bank, Martha Maeda (kulia).
0 comments:
Post a Comment