Misaada
ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25)
mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye
alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa
kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini
Mbeya.
Msamaria
mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye
nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi
za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es
salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight
Forwarders ya huko Uingereza.
Hivi
sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu
Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka
iwezekanavyo.
Kwa
niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa
shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo
aliouelekeza kwa mzazi huyo. Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia
misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila
kona ya dunia.
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na:
issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com nasi tutafikisha ubani wako. Serengeti Freight wametoa ofa ya kusafirisha bure misaada ya aina hii ASANTENI SANA
Michuzi Blog/Mbeya Yetu Blog
|
Misaada
kwaajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya
Momba, Mkoa wa Mbeya mara baada ya kufikishwa katika makao makuu ya
Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure toka
Uingereza na Wazee wa Kazi Serengeti Freight. |
Aida Nakawala 25
mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni
alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa
kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika
Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira
ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya
Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya
Wengi.
0 comments:
Post a Comment