Namelok
akimkabidhi msaada wa blanketi kwa mratibu wa kituo cha watoto
walemavu Monduli Mireile Kapilima katikati ni Katibu wa UWT Mkoa wa
Arusha Stamili Dendegu
Na Pamela Mollel,Monduli
Mbunge wa viti
maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine ameitaka jamii kujitolea
kuwasaidia watoto walemavu wanaolelewa katika kituo cha huduma ya
walemavu cha kanisa katoliki jimbo kuu Arusha kwa kuwa wazazi wengi
hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu
Alisema hayo jana
wilayani Monduli wakati akikabidhi misaada mbalimbali huku akiungwa
mkono na wanawake wenzake waliomsindikiza kuwaona watoto wenye ulemavu
wa viungo na utindio wa ubongo
Namelok alisema
kuwa kuna baadhi ya wazazi ambao hawana uwezo wa kumudu kulipa shilingi
1500 kwa siku hivyo ni vyema jamii ikaguswa kuwasaidia watu wenye
uhitaji
“Zipo familia
zinatumia zaidi ya shilingi 1500 kwa siku kila mmoja akijitolea
itasaidai kwakuwa kwa mwezi ni shilingi elfu 45000 kwa mtoto
mmoja”alisema Namelok
Pia mbunge huyo
alitoa shukrani zake kwa Mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa kwa kuweza
kutoa eneo hilo na kujengwa kituo chenye uwezo wa wawahudumia watoto
52.
Misaada aliyokabidhi Mbunge huyo ni pamoja na Blanket 50, shuka,unga,mchele,sabuni, sukari na mafuta
Mratibu wa kituo
hicho Mineile Kapilima alisema kituo hicho kimekuwa kikikabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ufadhili wa kudumu hivyo
mahitaji ya kituo kuongezeka siku hadi siku kwa kuwa awali kituo
kilikuwa kunauwezo wa kulaza wototo 30 lakini kwa sasa wanafika hadi 52
“ukosefu wa chakula,matibabu,nguo,hatuna ufadhili wa kudumu kwa kuwa wazazi wengi hawana hawana uwezo”alisema Kapilima
0 comments:
Post a Comment