Na
Magreth Kinabo
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid amesema
zaidi ya 35,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa
saratani.
Kauli
hiyo imetolewa leo na waziri huyo wakati akitoa tamko kuhusu
Siku ya Saratani Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka
Februari 4 kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Aidha
Dk. Rashid katika kuaadhimisha siku kutoa upimaji Februari 4 na 5,
mwaka huu bure, hivyo aliitaka jamii kujitokeza mapema ili
kupima ugonjwa huo.
Alisema
huduma za ugonjwa huo ni haki ya kila mtu na matibabu
yake ni bure.
“Hapa
Tanzania tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka. Kila
mwaka jumla ya wagonjwa wapya wa Saratani 44,000 hugundulika na zaidi ya 35,000
hufariki kutokana na ugonjwa huu,” alisema Dk. Rashid.
Aliongeza
kuwa takwimu za Taasisi ya Saratani Ocean Road, zinaonyesha kwamba kila mwaka
inapokea wagonjwa wapya wa Saratani 5,000. Wagonjwa hao wanakuja wakati
Saratani ikiwa katika kiwango cha juu - yaani hatua ya 3 na 4; na inasababisha uponaji
wake kuwa mgumu.
Kauli
mbiu ya maahimisho ya siku ya Saratani kwa mwaka huu ni “Kupunguza
unyanyapaa na kuondoa dhana potofu kuhusu Saratani”.
Aidha
Dk. Rashid alisema saratani inayoongoza hapa nchini kwa wanaume ni
Saratani ya Kaposi na Saratani ya Tezi Dume imekuwa ikiongezeka , na wanawake,
Saratani ya Shingo ya Kizazi.
Serikali
katika kuboresha imeanzisha huduma hizi katika Hospitali ya Bugando, baadae itaanzishwa
katika Hospitali za Rufaa za KCMC na Mbeya.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Twalib Ngoma
alisema utafiti uliofanywa unaonesha kuwa
tumbaku huchangia wagonjwa wa saratani kwa asilimia 40 .
0 comments:
Post a Comment