Baadhi ya madini
ya Tanzanite ambayo yanapatikana katika mabanda mbalimbali katika maonesho ya
53 ya Kimataifa ya Bangkok Gems and Jewelry Fair.
Mwenyekiti wa
Madini ya Viwandani Bw. Kassim Iddi Pazi, akimwonesha mgeni madini ya Ruby. Kutokana
na maelezo ya Bw. Pazi, ameeleza kuwa, madini hayo yametoka katika maeneo ya
Winza Dodoma na Matombo Morogoro.
Mfanyabiashara wa
Madini kutoka Kampuni ya Tom Gems Bw.Benjamin Mtalemwa akimwonesha mgeni madini
mbalimbali alipotembelea banda la Tanzania. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni
Mthamini wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Edward Rweymamu, Wa
pili kulia ni Afisa Madini kutoka Shirika la Madini Tanzania (STAMICO). Bw.
Peter Maha, na wa kwanza kulia ni Afisa toka Wizarani Bibi. Margareth
Muhony.
Na Asteria Muhozya,
Bangkok
**********
Madini
ya Tanzanite yamekuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya‘’Bangkok
Gems and Jewelry Fair’’, yanayoendelea katika eneo la kibiashara la ‘Impact
Challenger’, jijini Bangkok.
Madini
ya Tanzanite yanayozalishwa nchini Tanzania pekee duniani, yamekuwa
kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea
maonesho hayo ikiwemo wauzaji, wanunuzi
na wafanyabiashara ambao wamefika katika
banda la Tanzania kutaka kuona Tanzanite halisi kutoka Tanzania.
Aidha,
pamoja na kwamba madini ya Tanzanite yanazalishwa na Tanzania pekee, lakini katika maonesho hayo ya
Bangkok, madini hayo yanapatikana kwa kiasi kikubwa katika mabanda ya washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani jambo ambalo linaonesha namna madini
hayo yalivyo na muhimu katika sekta za kibiashara
na kiuchumi.
Akizungumzia
suala la uwepo wa madini ya Tanzanite
kwa kiasi kikubwa katika soko la kimataifa, na katika maonesho hayo, Kamishna Msaidizi
wa Madini , Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hamis Komba, ameeleza
kuwa, uwepo wa Tanzanite katika soko la
kimataifa unaashiria mahitaji makubwa ya madini hayo duniani na umuhimu wake
katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa
Tanzania, na nchi nyinginezo ikiwemo thamani yake katika soko la kimataifa na
upekee wake.
Aidha,
, aliongeza kuwa, hiyo ni changamoto katika
uthibiti wa madini hayo katika soko la kimataifa kutokana na uwiano wa takwimu za kiasi cha madini kinachotoka kwa kufuata
taratibu za usafirishaji madini hayo nje ya nchi na uwingi halisi unaoonekana katika soko la Kimataifa.
“Uwiano
wa takwimu za uzalishaji Tanzania na idadi halisi ya madini iliyopo katika maonesho
ya kimataifa ni tofauti. Hii ni changamoto
katika udhibiti wa madini haya” Amesema Kamishna Komba.
Hivyo,
ameongeza kuwa, Serikali inalifanyia kazi suala hili kwa lengo la kufanikisha usimamizi
na biashara endelevu ya madini ya Vito na usonara.
Mbali
na madini ya Tanzanite kuwa kivutio, katika
banda la Tanzania, vinyago vinavyotengenezwa kutokana na mawe aina
ya Zoisite, Basalt, Limestone,
Travertine, Granite na White marbale yanayopatikana Tanzania ambayo
yametengenezwa mapambo mbalimbali ya majumbani yamekuwa kivutio kikubwa
katika maonesho hayo kwa wageni waliotembelea banda la Tanzania kutoka nchi za
Ulaya na Asia, akiwemo pia Rais wa
Shirikisho la wafanyabiashara wa vito na usonara Bw. Somchai Phornchindarak,
ambaye pia alitembelea Banda la Tanzania na kuonesha kuvutiwa na kushangazwa na
mapambo hayo.
Akizungumzia
kuhusu ushiriki wake katika maonesho hayo, Mratibu wa kituo cha Tanzania
Geomological Center, Bw. Musa Shanyangi, amesema kuwa, maonesho hayo yamekuwa
ya manufaa katika soko la madini ya mawe kutokana na wageni wengi kuonesha
kuvutiwa nayo.
Shanyangi, ameongeza kuwa, tayari kituo hicho kimeanza kufanya ukarabati wa
miundombinu na kuandaa mitaala ya
kufundishia , hivyo chuo kitaanza kutoa mafunzo ya uchongaji wa vinyago,
ukataji wa madini ya vito, uchongaji wa
mawe, mafunzo ya utambuzi wa madini ikiwemo pia maabara itakayotumiwa kwa ajili
ya shughuli hizo.
Hivyo,
amewataka vijana wa kitanzania kuitumia fursa hiyo kupata mafunzo hayo ili
waweze kuingia katika sekta ya madini
kwa kuwa itawasiadia kujiajiri, kuinua vipato vyao na kuchangia katika ukuaji
wa uchumi. Aidha, amewataka wadau katika sekta ya madini kuona umuhimu wa
kuongeza thamani ya madini.
“
Maonenesho hayo, yamekuwa na manufaa kwa Tanzania, kituo chetu kimepata fursa ya kufaa kwa bidhaa za mawe, kwasababu nimejaribu
kuzunguka katika mabanda mengi sana sijaona bidhaa kama hizi. Hiyo ni fursa kwetu
na kwa vijana wa Tanzania katika soko hili. Amesema Shanyangi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Madini ya Viwanda Tanzania (FEMATA), Bw. Kassim Iddi
Pazi akielezea ushiriki wake katika
maonesho hayo na soko la madini kimataifa ameeleza kuwa, maonesho hayo
yamefungua fursa kubwa ya biashara kutokana na kupata oda nyingi za madini mbalimbali yakiwemo madini ya ruby na zoisite.
Ameongeza
kuwa, wamegundua mambo mengi ya muhimu yatakayowasaidia wachimbaji katika sekta
hiyo na hasa madini ya viwandani.
“Hakuna
kitu muhimu kama kushiriki maonesho. Ruby yetu ni bora na imependwa sana hapa.
Wengi walijua Ruby inatoka Bama lakini uwepo wetu umewafanya kujua Ruby safi
inatoka Tanzania. Namshukuru Sana Mhe. Rais na Wizara kwa kutuwekea mazingira
mazuri katika sekta hii na kutuwezesha kushiriki maonesho haya”. Amesema, Pazi.
Aidha,
ameongeza kuwa, kama viongozi wa shirikisho hilo, wanao wajibu wa kuwasaidia
wachimbaji wengine kupata taarifa mbalimbali kuhusu sekta hiyo kutokana na
uzoefu walioupata na hivyo amewataka kufanya kazi na Serikali kwa ushirikiano.
Tanzania
inashiriki kwa mara ya kwanza maonesho hayo ya 53 ya Kimataifa ya ‘Bangkok Gems
and Jewelry Fair, ambapo mwaka 2013 ilishiriki kama nchi mwalikwa ambapo kiongozi
wa ujumbe wa Tanzania alikuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini
anayeshughulikia Nishati Mhe. Stephen Masele.
0 comments:
Post a Comment