Halmashauri aya Jiji la Arusha imevunja nyumba zake338 baada ya kushinda kesi iliyofunguliwa na wapangaji Sangito
Sumari na wenzake 216 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha.
Operesheni hiyo inayojulikana kama “Operesheni Mongela”ilianza
saa 12 asubuhi jana kwa kuvunja nyumba 56 eneo la Kilombero, nyumba 198 eneo la
Kaloleni na nyumba 84 katika eneo la Themi.
Wengi walitegemea kuibuka vurugu wakati wa uvunjaji nyumba lakini
hadi mchana hapakuwa na pingamizi kwa wapangaji badala yake wenyewe walihamisha
vitu vyao mapema jana asubuhi kabla ya zoezi la kuvunja kuanza.
Hata hivyo kuvunjwa kwa nyumba hizo kumeleta neema kwa baadhi
ya watu wakiwamo vijana wanaokusanya vyuma chakavu kuvamia maeneo hayo na kuokota
kila aina ya chuma au kitu ambacho waliamini kinaweza kuuzwa na kuwapatia
fedha.
Akiwa eneo la Kaloleni baada ya kukamiliza kuvunjwa nyumba za Kilombero, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mongela
alisema, ‘Operesheni Mongela’ ilipata baraka zote za viongozi wa Serikali wanasiasa
wakiwamo madiwani wote Mbunge na Meya wa Jiji.
0 comments:
Post a Comment