Rais Jakaya Kikwete (kuli) akiwa pamoja na Marais Wastaafu wa Tanzania, Benjamini Mkapa (kushoto) na Mzee Ali hassani Mwinyi wakati wa hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa
watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya
kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/-
zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22,
2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
*********
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
usiku wa jana, Jumamosi, Februari 22, 2014, aliongoza harambee ya
kupatikana kwa zaidi ya sh milioni 600 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya
kisasa vya matibabu kwa ajili ya Wodi ya Watoto katika Hospitali ya
Taifa, Muhimbili, Dar Es Salaam.
Katika
halfa hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Dar Es Salaam,
Rais Kikwete pia ameahidi kuendeleza kuongoza jitihada za kupatikana kwa
kiasi cha sh milioni 328 ambazo zinahitaji kukamilisha hesabu ya sh.
929, 915,000 ambazo ndizo zilikuwa lengo la halfa ya jana.
Halfa hiyo pia iliwakutanisha viongozi wakuu wa awamu tatu za uongozi wa
juu wa Tanzania ambako Rais wa Pili wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi
na Rais wa Tatu za Tanzania, Mzee Benjamin William Mkapa walikuwa
wenyeji wa halfa hiyo kwa nyadhifa zao kama walezi wa Chama cha
Madaktari wa Watoto Tanzania (PAT).
Uchangiaji
katika halfa hiyo ulikuwa wa aina tatu – kuna fedha taslimu milioni
55.4 zilizochangwa moja kwa moja, kuna ahadi za uchangiaji na kuna
wachangiaji walioamua kuwa watatoa fedha za kununua vifaa mbali mbali
vinavyohitajika katika Wodi hiyo ambayo gharama yake inakadiriwa kufikia
dola za Marekani 570,500.
Katika
halfa hiyo, Ikulu ya Rais Kikwete imetoa mchango wa kununua mashine
iitwayo Infant Radiant Warmer yenye thamani ya dola za Marekani 15,300
wakati Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mama
Salma Kikwete imechangia ununuzi wa mashine iitwayo Compressor Nebulizer
ambayo gharama yake ni dola za Marekani 12,000.
Rais wa Chama cha Madaktari wa
Watoto Tanzania (PAT), Rodrick Kisengeakizungumz wakati wa harambee hiyo ambayo iliandaliwa nao.
Mlezi wa PAT Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa akizungumza.
Waalikwa katika hafla hiyo wakifuatilia matukio.
Mkurugenzi wa Redio One, Deo Rweyunga akitamka kwa niaba ya Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi ahadi yake.
Deo Rweyunga akipeana mkono na Rais Jakaya Kwete baada ya kutoa ahadi ya Mengi ya shilingi za kitanzania zaidi ya Milioni 100.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo akipeana mkono na Rais Jakaya kiwete baada ya kutoa ahadi ya Mamlaka hiyo.
Benki ya Posta Tanzania (TTB) nao waliangusha ahadi yao
Rais
Jakaya Kikwete akipokea hundi yenye thamani ya sh. Milioni kumi kutoka kwa
Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu,
wakati wa hafla ya kuchangia maboresho ya matibabu ya watoto katika hospital ya
Taifa Muhimbili Dar es Salaam jana. Katikati ni Rais wa Chama cha Madaktari wa
Watoto Tanzania (PAT), Rodrick Kisenge na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harison
Mwakyembe. Jumla ya shilingi milioni 602 ziliahidiwa.
Mkurugenzi wa Mfumo wa Mawasiliano wa PPF, Robert Mtendamema akikabidhi mfano wa hundi kwa rais.
Mfano wa kuigwa; Mkurugenzi wa CXC Safaris & Tours, Charles Hamkah, akikabidhi mchango wake.
0 comments:
Post a Comment