Mkuu
wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Mjema akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu habari za upotoshaji
zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku na baadhi ya mitandao ya
kijamii kuhusu chuo hicho, leo jijini Dar es salaam.
Na.
Aron Msigwa – MAELEZO.
Mkuu
wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es salaam Prof. Emanuel
Mjema amesema kuwa habari zilizoandikwa
na kuchapishwa na gazeti moja la kila siku na baadhi ya mitandao ya kijamii hapa
nchini zililenga kukidhalilisha chuo na kuipotosha jamii kufuatia chuo hicho kuendelea
kufanya vizuri katika kulinda maadili na viwango vya taaluma hapa nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mkuu wa chuo hicho amesema kuwa
habari zilizochapishwa kuhusu kuwekwa kwa mfumo wa kamera za kisasa madarasani na taarifa ya kufukuzwa kwa mwalimu
mmoja wa chuo hicho akihusishwa na vitendo vya ngono na wanafunzi zimepotoshwa
na vyombo hivyo kwa kukosa weledi wa kushindwa kupata uhalisia na usahihi
wa habari husika kutoka mamlaka za chuo hicho.
Prof.
Mjema amesema kuwa Chuo cha Elimu ya Biashara ni Chuo cha Serikali ambacho kimekua
kikitoa Elimu ya Biashara kwa miaka 49 na kuongeza kuwa chuo hicho kinaajiri
wakufunzi wake kupitia utaratibu wa serikali wa kutangaza nafasi za kazi
kupitia Tume ya Ajira iliyopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa umma.
Ameongeza
kuwa chuo hicho kina wakufunzi na wataalam wanaoheshimu maadili ya utumishi wa
umma na taaluma zao na kuongeza kuwa chuo hicho kina wakufunzi wenye sifa ambao
hawahitaji kufuatiliwa na mtu katika kazi zao.
“Nachopenda
kusema ni kwamba chuo chetu sasa kinao wataalam na wakufunzi wenye sifa na
walioajiriwa kwa kuzingatia kanuni na vigezo vilivyowekwa,taarifa zilizotolewa
hazina ukweli wowote na zimelenga kukidhalilisha chuo na kuipotosha jamii”
Amesema
kuwa kamera za kisasa ziilizofungwa
katika vyumba vya madarasa vya chuo hicho zimewekwa kwa lengo la kudhibiti
udanganyifu katika mitihani na kuimarisha ulinzi na usalama wa mali za chuo na
kuongeza kuwa juhudi zinafanyika katika mwaka ujao wa fedha kuongeza vifaa
hivyo hasa katika maeneo ya kuingilia nay ale yanayotumiwa na watu wengi chuoni
hapo.
“Napenda
kuwafahamisha kuwa kamera za CCTV tulizonazo zimefungwa katika vyumba vya
madarasa kulingana na teknolojia iliyopo sasa na ni jambo la kawaida na zimefungwa
kwa lengo la kuimarisha ulinzi kwa lengo la kutoa wataalam waliobobea na si kama
ilivyoandikwa kwa kupotoshwa na gazeti hilo na baadhi ya mitandao ya kijamii
kuwa zinalenga kudhibiti vitendo vya ngono darasani” amesema Prof. Mjema.
Aidha
kuhusu hali ya ulinzi na usalama chuoni hapo amesema kuwa chuo hicho kimekuwa
na utaratibu wa kuweka walinzi getini kwa miaka 49 na kuongeza kuwa hakuna
walinzi wapya walioajiriwa kwa ajili ya kukagua mavazi ya wanafunzi hao
huku akibainisha kuwa utaratibu uliopo sasa wa kukagua vitambulisho kwa
wanafunzi wanaoingia chuoni hapo na wageni wengine wanaoingiia ni wa kawaida
kwa ajili ya usalama wa chuo.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa chuo hicho amesema kuwa chuo hicho kitaanza kutoa masomo
ya juu kwa ngazi ya shahada za uzamili kuanzia
mwaka ujao wa kitaaluma na kutoa wito kwa wananchi kuichangamkia fursa hiyo.
Pia
amesema kuwa chuo hicho kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha “Eastern Finland” kitaanza kutoa shahada za
umahiri na kufafanua kuwa wataalam wa kuifanya kazi hiyo hapa nchini wapo.
“Tutaanza
kutoa mafunzo kwa ngazi ya shahada za uzamili katika mwaka ujao wa kitaaluma,
wahadhiri wanaofundisha sasa hapa chuoni wana elimu za juu hivyo kuwezesha
mchakato huo kuanza”
Katika
kuboresha kiwango cha elimu chuoni hapo Prof. Mjema ameeleza kuwa Chuo chake tayari kimeingia mkataba na chuo Kikuu cha
masuala ya Teknolojia cha Shenyang , kilichopo nchini china ambapo wanafunzi wa
vyuo vya CBE nchini wataweza kwenda China kumalizia masomo yao kwa mfumo wa
kubadilishana.
“
Ni hatua nzuri katika maboresho ya elimu katika chuo chetu kwa kushirikiana na
vyuo vya nje hasa Finland na China na sasa baadhi ya wanafunzi wameshaanza
kunufaika” ameeleza Prof. Mjema.
0 comments:
Post a Comment