Abiria
wa treni iliyokwama Dodoma wakiwa na watoto wao wakipata chochote
wakati wakisubili hatima yao huku katika stesheni hiyo kukiwa
hakutamaniki kwa uchafu unaotishia afya zao kutokana na abiria zaidi ya
1500 kutakiwa kutumia matundu manne ya vyoo.(Picha na John Banda)
Wasafiri
wa treni toka Kigoma na Mwanza kuelekea Morogoro na Dar es laam wakiwa
wamelala kwenye mabehewa hawajui cha kufanya baada ya treni hiyo
kushindwa kuondoka Dodoma kutokana na Maji kujaa relini Gulwe na
Mzaganza.
Abiria
waliokuwa wakisafiri na treni kuanzia kigoma kwenda Dar es laam
wakielekea kwenye ofisi ya mkuu wa stesheni ya Dodoma mara baada ya
treni hiyo kukwama kuondoka kwa sababu ya mafuliko yaliyosababishwa na
mvua maeneo ya Gulwe na Mzaganza.
Abiria wakisongamana dirishani kupokea fedha za kujikimu 3500 zilizotolewa na shirika la reli baada train hiyo kukwama kuondoka Dodoma.
Abiria hao wakiwa kwenye foleni kuelekea kwa mkuu wa stesheni ya Dodoma,
Zacharia Kilombele ambako walikuwa wanapewa pesa ya kujikimu tsh. 3500 kwa abiria zaidi ya 1500 walikwama kutokana na mafuriko.
CHANZO: PAMOJA BLOG
0 comments:
Post a Comment