Uwezonineno
la Kiswahili lenyemaanaya ‘kipawa au umahiri’. Uwezo ni mradi wa miaka minne wenyelengo
la kuboresha ujuzi katika kusoma na kuhesabu miongoni mwa watoto wenye umri wamiaka
6-16 nchini Kenya, Tanzania na Uganda, wakutumia njiabunifu kwenye kuleta mabadiliko
ya kijamii ambayo yanatokana na raia wenyewe na kuwajibika kwa umma.
Kwa mwaka huu
zoezi la upimaji limeanza hivikaribuni .Hapa kunabaadhi ya picha za matukio ya zoezi
la upimaji manispaa ya Singida.
Faiza Ramadhani,
mwanafunzi wa darasa lasita, shule ya Msingi Misufini, Manispaa ya Singida, akifanya
jaribio la kusoma kamasehemu ya zoezi la upimaji wa stadi KKK. Wanaomuongoza ni Winfrida Makelele (kushoto) na Samwel Msihi
(kulia) kutoka shirika la Uwezo.
Mkazi wa mtaawa Mitunduruni,
ManispaayaSingida, Mwanahamis Ali Sembo (kushoto) akitoa maelezo ya kaya
yakekwaHadra Mohamed, mkusanyataarifawashirika la Uwezo.
Hadija Ramadhani,
mwanafunzi wa Darasa la Nne, Shule ya Msingi Mitunduruni, ManispaayaSingida akifanya
jaribio la kupima stadiza KKK linaloendeshwa na shirika la Uwezo.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Kindai, Bw. Athman Masudi Maganga (kushoto) akisikiliza maelezo juu ya
matumizi ya dodoso la upimaji wa stadiza KKK, kutoka kwa Mratibuwa Uwezo Wilaya
(Manispaa ya Singida), Bibi ZuhuraKayra (kati). Aliyeupande wa kuliani Bi.
Shamim Hatibu, mkusanya taarifa wa Uwezo, Mtaa wa Kindai, Singida Manispaa.
0 comments:
Post a Comment