Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion inayoandaa tamasha la Krismas Bw. Alex Msama amezungumza na waandishi
wa habari leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam na kuelezea
maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika siku ya sikukuu ya Krismas kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa
injili kutoka ndani na nje ya Tanzania ametaja nchi ambazo washiriki watatoka
kuwa ni Tanzania yenyewe, Afrika Kusini, Nigeria, Zambia, DRC Congo, Kenya,
Uganda, Burundi na Rwanda.
Ameongeza kuwa mmoja wa waimbaji hao kutoka
Zambia natatarajia kuzindua albam yake mpya katika tamasha hilo. Msama pia
amesema nusu ya fedha zitakazopatikana zinatarajia kulipia karo za shule kwa
watoto wasiojiweza wapatao 300 na fedha nyingine zitaelekezwa kwenye ujenzi wa
kituo cha misaada kwa w asiojiweza kitakachoitwa Jakaya Mrisho Kikwete Rafiki
wa wasiojiweza kinachotarajiwa kujengwa huko Pugu, Kauli Mbiu ya Tamasha hilo
ni "TANZANIA NI YA WATANZANIA TUILINDE NA KUIDUMISHA AMANI
YETU"
0 comments:
Post a Comment