Nafasi Ya Matangazo

November 11, 2013

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO), Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa.

Taarifa ya Mwandishi wa habari Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga imeeleza kuwa Katika uteuzi huo, Rais amemteua Prof. Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO).

Rais pia amemteua Bwana Freddy Safiel Manongi kuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ambaye hivi sasa ni kaimu Mkuu wa Chuo cha Wanyamapori cha Mweka na pia amemteua Prof. Audax Zephania Philip Mabula kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa.

Uteuzi huu umeanza rasmi mwishoni mwa Mwezi Octoba mwaka huu.
Posted by MROKI On Monday, November 11, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo