Askofu
Damian Dallu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita akiongoza ibada ya
mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu
Dkt. Sengondo Mvungi katika makaburi ya familia kijijini Chanjale wilaya
ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Mke wa
aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt. Sengondo
Mvungi, Bi. Anna Mvungi akiweka shada la maua katika kaburi la mume
wake wakati wa mazishi kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani
Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Waziri
wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James
Mbatia wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi wakati wa mazishi kijijini
Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18,
2013.
Jeneza
lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt.
Sengondo Mvungi likishushwa kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika
kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba
18, 2013.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, mkewe Mama Tunu, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba Jaji Joseph Warioba na viongozi wengine wakifuatilia ibada ya
mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt.
Sengondo Mvungi. Mazishi hayo yalifanyika kijijini Chanjale wilaya ya
Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.
Familia
ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo
Mvungi ikifuatilia ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijijini cha
Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Askofu
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha Josephat Lobullu (kulia) na
Askofu wa Jimbo la Same Rogath Kimaryo wakiongoza ibada ya mazishi ya
aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi.
Ibada hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chanjale wilayani Mwanga mkoani
Kilimanjaro na kuhudhuriwa pia na Askofu Damian Dallu (katikati) wa
Jimbo la Geita JUmatatu, Novemba 18, 2013
0 comments:
Post a Comment