TUKIO la shambulizi la risasi lililotokea hii
leo asubuhi Ilala Amana jirani na Hoteli ya MM na Klabu maarufu ya wazee
limesababisha vifo vya watu wawili na kuacha majeruhi watatu wawili kati yao
wakiwa taabani.
Taarifa za awali za Polisi zinapasha kuwa, Watu
walio poteza maisha katika tukio hilo ambalo lilikuwa ni la mtu aliyetambulika
kwa jila la Godfrey Munisi kuwapiga risasi wana familia lilisababisha kifo cha
Alfa Alfred na liliwajeruhi Francis Khiranga Shumira , Christina Alfred, Hellen Elieza Newa.
Taarifa hizo zinasema kuwa Mfyatua risasi huyo
ambaye baade alijiua nayeye, Godfrey Munisi alikuwa na uhusiano wa karibu na
Christina Alfred Newa.
Katika tukio hilo, ambalo linaelezwa kuto tofautiana
sana na lile la Mwanahabari ufoo Saro lililotokea miezi ya hivi karibuni,
muuaji alimjeruhi Nshumila kifuani na
mama yake Christina alijeruhiwa maeneo
ya begani na hali zao siyo nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Huku Christina akijeruhiwa mkononi na mguuni
ambapo alitibiwa katika Hospitali ya Amana na Kuruhusiwa kurudi nyumbani huku mdogo
wa Christina, Alfa Alfred akifariki kabla ya kufikishwa Hospitali.
Marehemu Alfa Alfred Newa pia alikuwa wa benki ya Barclays ya jijini Dar es Salaam. Shumira ni baharia kitaaluma na inaelezwa kuwa ni raia wa Kenya.
Mapema
leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala
Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu
wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa
limetokana na wivu wa kimapenzi.
Dereva mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu nyingine.
Kwa mujibu wake dereva huyo aliendelea kusimulia, alimpeleka jamaa mpaka aneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM.
Mara baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba, aliendelea kusimulia dereva huyo.
Wakati jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari mama mmoja na wadada wawili.
Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Carol, hii ni kwa mujibu wa dereva huyo na mara baada ya kuona hivyo hivyo ikabidi akimbie.
Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia limpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu.
Mtuhumiwa na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.
Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauwaji hayo licha ya watu wengi ambao nilipata bahati ya kuongea nao wakilihusisha tukio hilo na mambo ya kimapenzi. SOURCE: DANCHIBO BLOG.

0 comments:
Post a Comment