Na
Andrew Chale
ONESHO la
Usiku wa Khanga za Kale 2013, maarufu kama ‘5th Extra Vaa Khanga Party’
linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam usiku wa Novemba 8, kwenye Hoteli
ya Serena na kupambwa na burudani ya nguvu kutoka kwa bendi ya Mashauzi
Classic.
Mwandaaji
wa onesho hilo, Asia Idarous Khamsin,
alisema jana tayari maandalizi yake yamekamilika na amewasihi wadau
kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo la aina yake kujionea mitindo
mbalimbali ya khanga.
“Wadau
wa mitindo nchini, watapata burudani na kufurahia mitindo ya khanga
itakayooneshwa kwenye shoo hiyo, hii si ya kukosa kwa mwaka huu,” alisema Asia
Idarous.
Alisema
usiku huo, vazi la khanga ndilo litakuwa
maalumu kwa wadau watakaohudhuria
sambamba na kupinga matumizi ya dawa za kulevya.
Onesho
la Usiku wa Khanga za Kale 2013, ambalo mwaka huu limeandaliwa kwa ushirikiano
wa Asia Idarous Khamsin na Fabak Fashions, linatarajiwa kuwa na shangwe
mbalimbali ikiwamo kushirikisha watu maarufu na mastaa mbalimbali.
Kuhusu
kiingilio, Idarous alisema kwa viti vya kawaida ni sh 30,000 na viti maalumu
itakuwa ni sh 50,000 na kuongeza kuwa tiketi zimeanza kuuzwa Fabak Fashions
Mikocheni na Gift Shop Serena Hoteli.
Alisema
onesho hilo linafanyika chini ya uwezeshaji wa wadhaminiwa kama bia ya Redd’s,
CXC, Clouds FM, Vayle Spring, Magic FM, Eye View, Amina Design, Kabile, Voice
of America, Origin Unite, Channel Ten, DTV, Times FM, Michuzi Media Group,
Event Light na Miss Tz.
0 comments:
Post a Comment