Nafasi Ya Matangazo

November 02, 2013

Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Dacico Diploma, Materego Materego, akiambaa na mpira kuelekea katika lango la Dacico Certificate, baada ya kumtoka kiungo mkabaji wa timu ya Dacico Certificate, Deogratias Deo Deo, katika mchezo wa kusaka kikosi cha kwanza cha timu ya chuo  uliofanyika katika Uwanaja Kibwegele Kibamba Dar es Salaam, timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana 1-1.(Picha na Mathias Haule). 
 **********
Na Mariam Mwakatumbula, DACICO
TIMU za mpira wa muguu za madarasa ya Diploma na Certificate za Chuo cha Uandishi cha  DACICO jana zimeshindwa kufungana baada ya kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 katika mchezo wa marudiano uliofanyika katika Uwanja wa Kibwegele uliop[o Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam

Wakicheza mbele ya Mkurugenzi mkuu wa Chuo, Idrisa Mziray, wachezaji wa timu zote walionekana kucheza kwa kukamiana kutokana na kila mmoja kutaka kuchaguliwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo ambayo inatarajia kumenyana na timu za vyombo vya habari zikiwemo timu za Taswa FC.

Aidha katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa chuo cha DACICO uliopo Kibamba CCM timu hizo zilishindwa kutambiana baada kumaliza dakika 90 kwa kufungana 2-2 na hivyo kuomba mchezo wa marudiano ambao pia timu hizo zimeshindwa kupata mbabe na kulazimisha kutafutwa mchezo mwingine ili iweze kujulikana ni timu ipi yenye ubavu itakayoweza kuibuka na ushindi.

Wakizungumza baada ya mpambano huo makocha wa timu zote mbili, Mwalimu Kashilima wa Diploma na Mwalimu wa Michezo wa Timu ya Certificate Ombeni  wamesema kuwa kushindwa kupata timu iliyoibuka na ushindi kumetokana na wachezaji kucheza kwa kukamiana na hivyo kusababisha mchezo huo kutawaliwa na vurugu zilizosababisha mwamuzi kushindwa kuumudu vyema mchezo huo kutokana na kila mara wachezaji kwenda kwa mwamuzi na kumzongazonga.

"Wachezaji wangu wamecheza mpira mgumu sana leo na hiyo imetokana na kukamia mpambano, unajua timu hizi ni pinzani pamoja na kwamba wanasoma katika chuo kimoja, kikubwa hapa ni kwamba wachezaji wa Diploma wanawaona hawa wa Certificate kama watoto wadogo, lakini kumbe mpira ama mchezo wowote hauna kuzarau, kwani hawa vijana wangu wa Certificate wanacheza mchezo mzuri na wa hali ya juu ila kwa leo naweza kusema wamecheza mchezo wa kuwaiga hawa wachezaji wa timu ya Diploma " alisema mwalimu wa michezo DACICO.

Wakati huo huo kocha wa Diploma,Kasilima amewalaumu wachezaji wa timu yake kwa kushindwa kulinda goli ambalo lilifungwa mapema kwenye dakika za mwanzo kabla ya kwenda mapumziko baada ya mchezaji nyota wa timu hiyo Hilary Mgenzi kuwalamba chenga walinzi wa timu ya Certificate na kisha kufunga kwa Shutin kali lililokwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda mlango wa Certificate othman juma akiutazama kwa macho.

"Tiu yangu ilicheza vyema, na tukapata goli mapema ila ni matatizo madogo tu ya kiufundi yametufanya tutoke suluhu na wapinzani wetu…pia mianya iliyowapa goli Certificate na kusawazisha,” alisema Kasilima.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Chuo, Idrisa Mziray, amesema mchezo wa marudiano umepangwa kufanyika mapema baada ya wanafunzi kumaliza mitihani ambayo inatarajia kuanza jumatatu ya kwanza ya mwezi huu.
Posted by MROKI On Saturday, November 02, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo