Muuguzi katika kituo hicho cha St. Laurent Diabetes Centre, akimpima Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ask. Dk. Alex Malasusa huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akishuhudia.
Wananchi mbalimbali wakipata huduma ya kupimwa ugonjwa wa sukari katika kituo hicho cha St. Laurent Diabetes Centre
Burudani kutoka Mjomba Band ikitolewa
******
Ugonjwa wa Kisukari umekuwa tishio kwa
mataifa mengi duniani, Tanzania ikiwemo. Inasemekana kuwa nchi maskini na
zinazoendelea duniani ndio zinazongoza kwa ugonjwa wa Kisukari. Aidha, kwa sasa
ugonjwa wa Kisukari unashika nafasi ya tatu duniani kueneza vifo.
Katika makala hii, Mtaalam wa Maradhi
ya Kisukari , Dkt. Mary Mayige , kutoka kituo cha Kisukari cha St.
Laurent Diabetes Centre, jijini Dar es Salaam anaeleza kwa ufasaha dalili za
ugonjwa huu, kinga na tiba yake.
Dkt. Mary Mayige anafafanua kuwa Kisukari kwa kifupi (na kwa
lugha ya kueleweka) ni ugonjwa unaotokana na kuwa na kiasi kikubwa cha sukari
kwenye damu.
Aliongezea kuwa sukari inapokuwa nyingi
kwenye damu ya binadamu, hapo ndipo mtu huyo husumbuliwa na maradhi hayo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kituo cha Kisukari yaani St. Laurent Diabetes Centre, Dkt.
Mary Mayige aliwakaribisha watanzania wote katika upimaji wa bure wa Kisukari
na pressure katika kituo chao kilichopo Msasani karibu na CCBRT, Dar es Salaam
tarehe 10/11/2013. Kabla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho, watanzania
walijitokeza kwa wingi kupima na kujua afya zao siku hiyo na kujipatia ushauri
wa bure kutoka kwa madaktari na wauguzi wa kituo hicho.
Watu wengi walinufaika na huduma
zilizotolewa na kitu hicho cha St.Laurent Diabetes Centre.
Siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya Kisukari
Duniani, kituo cha St. Laurent Diabetes Centre walifanya uzinduzi rasmi wa
kituo chao Wakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Dkt. Alex
G. Malasusa, pamoja na Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii, Dkt .Hussein Mwinyi, na
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba na
waheshimiwa wageni waalikwa wawakilishi kutoka serikalini, kwenye sekta binafsi , za umma na sekta za afya.
0 comments:
Post a Comment