Nafasi Ya Matangazo

November 06, 2013



Benki ya Barclays Tanzania, Leo hii Imezindua Rasmi Kampeni ijulikanayo kama “Ongeza Akiba Yako” kwa wateja wake. Kampeni hii ilizinduliwa Mnamo Tarehe 16, Septemba, 2013, na inatarajiwa kuendelea Mpaka Tarehe 16, Januari, 2014.

Kampeni hii itawapa fursa wateja watano, (5) kila mwezi, kujishindia mpaka kiasi cha shilingi za kitanzania Milioni moja kwa kila mmoja katika kipindi chote cha kampeni. Droo ya kampeni itakuwa ikifanyika katika kila wiki ya mwisho wa mwezi, ikiangalia vigezo vya kila mteja.

Akiongea na waandishi wa Habari leo hii, Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wa kawaida, Bwana Musa Kitoi alisema, “Kampeni hii iko wazi kwa wateja wote wa Benki ya Barclays, na wale wapya, kupitia akaunti zao mbali mbali za fedha za Tanzania. 

Kwa mteja kujipatia nafasi ya kushiriki, mteja anapaswa kutokushuka chini ya kiwango cha shilingi Laki Tatu (300,000). Kiwango hiki kinatakiwa kiwekwe ndani ya mwezi toka kampeni izinduliwe, na kinatakiwa kisishuke kiwango kilichotajwa.

Wateja wapya wanaweza kuingia kwenye droo hii pindi tu watakapofungua akaunti zao, na kuweka kiwango kisichopungua shilingi laki tatu. Baada ya kufungua akaunti, na kuweza kubakisha kiwango kilichotajwa kwenye akaunti, wateja, (wa zamani na wapya) wataingizwa kwenye droo ya kila mwezi, na wateja watano (5) watapata bahati ya kuongezewa mara mbili akiba zao, na katika droo kubwa ambayo itakuwa mwisho wa kampeni, mshindi atajinyakulia kiasi kipatacho milioni thelathini, (30,000,000)”.

Aliendelea na kusema, “Leo hii tutapata washindi wetu wa kwanza  watano (5) wa kampeni hii, na Benki ya Barclays inawapongeza wote waliojishindia, na kuwasihi wateja wote kushiriki katika kampeni hii, wakati tukikaribia kipindi cha sherehe za mwisho wa mwaka”.

Posted by MROKI On Wednesday, November 06, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo