Nafasi Ya Matangazo

November 06, 2013

 
 Mfanyakazi wa TBC , Ramadhan Gize.
Mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Ramadhan Gize ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosaidiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo katika eneo la Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea baada ya watu hao kuvamia duka moja katika eneo la Ubungo Maziwa kwa lengo la kupora, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwajabu Rajabu amejeruhiwa kwa kupigwa risasi. 

Marehemu Gize alikuwa dereva katika shirika hilo na msiba upo Ubungo, Msewe jijini Dar kwa wazazi wake ambako mipango ya mazishi inafanyika. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!
Posted by MROKI On Wednesday, November 06, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo