Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu na kiongozi wa Taasisi ya Tanga Women Development Initiative (TAWODE) wakizundua mradi huo.
Watoto wakike ambao ndio walengwa wa mradi huo wakiwa na vyeti vyao.
Watoto wa Kike wakifuatilia uzinduzi wa taasisi yao.
Moja ya vipeperushi
OKTOBA 11 ya kila mwaka ni siku ya mtoto wa kike
duniani. Mkoani Tanga waliadhimisha siku hiyo ya mtoto wa kike kwa
kuzindua mradi maalum wa kuwajengea uwezo wasichana wa mkoa wa Tanga chini ya
Taasisi ya Tanga Women Development Initiative (TAWODE).
Mgeni rasmi katika uzinduzo huo uliofanyika
uwanja wa michezo wa Mkwakwani alikuwa Mhe Chiku Galawa, Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
na kuhudhuriwa pia na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga, ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Tanga wakiongozwa na Halima Dendegu .
Akizungumzia uzinduzi huo Naibu Waziri mwenye
dhamana hiyo ya Jinsia, Ummy Mwalimu alisema kuwa amefurahishwa sana na
uzinduzi wa mradi huo.
“Kupitia mradi huu ninafurahi kuona nikitekeleza
kwa vitendo dhamira yangu kama kiongozi - 'niliechaguliwa' na wanawake wa mkoa
wa Tanga- kuchangia kuboresha maisha ya Wanawake na Watoto wa Mkoa wa Tanga”,
alisema Mwalimu.
Pia shukrani zilienda kwa Balozi wa Denmark nchini,
Johnny Flento kwa kuunga mkono jitihada hizo.
Mradi huo utatekelezwa ktk Wilaya za Pangani,
Muheza, Mkinga, Lushoto na Tanga Mjini, umelenga kuchochea uwezo na ubora wa
wasichana (wa umri wa miaka 10-24), kutambua weledi na umuhimu wao kwa
maendeleo yao na ya jamii zao.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa alisema kuwa
kupitia mradi huo Mkoa umedhamiria kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wasichana
waliopo katika shule za Serikali za Msingi na Sekondari, kuboresha hali ya afya
ya uzazi, kupunguza mimba za mapema, ndoa za utotoni na maambukizi ya VVU.
“Tumepanga kuwafikia moja kwa moja wasichana
16,000 na zaidi ya 100,000 kupitia njia mbalimbali ikiwemo mabango, Radio
jingles (Mwambao FM 106.0), matamasha ya wasichana na njia nyingine mbalimbali,”alisema
Galawa.
Aidha Wasichana 1,000 waliopo shuleni na
wanaoishi ktk mazingira magumu wataingizwa katika Mfuko wa Bima ya afya ili
kuweza kupata huduma za afya bure.
Endapo jitihada hizo
zitazaa matunda zitachochea maendeleo ya wanaTanga ambao wamekuwa na utayari wa
kupokea ushauri na mawazo ya wadau mbalimbali juu ya Utekelezaji mzuri wa Mradi huo.
0 comments:
Post a Comment