Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akiowaonyesha Makatibu Wakuu wa Vyama vilivyopigania uhuru wa nchi zao barani Afrika na ujumbe wa chama cha Kikomunisti cha China CPC wakiangalia ngoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli nje kidogo ya Manispaa ya Iringa.
Baadhi ya majengo mabweni madogomadogo yanavyoonekana kwa juu eneo lenyewe linavyoonekana
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribisha wageni wake mara baada ya kufika katika kambi ya Ihemi mkoani Iringa leo kutoka kulia ni Obed Papela kutoka ANC na Naibu Waziri ,Didymas Mutasa Katibu MKuu wa chama cha ZANU- PF cha Zimbabwe, kutoka kushoto ni Dino Matrose Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA cha Angola na mwenye shati jeupe ni Filipe Paunde Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO cha Mozambique na mkalimani wake.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimuonyesha eneo hilo Ai Ping aliyevaa kofia Naibu Waziri wa mambo ya Nje wa China kutoka chama cha Kikomunisti cha China CPC ukubwa wa eneo hilo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Billy Masetlha Mjumbe wa Kamati kuu na Mahusiano wa Chama cha ANC Cha Afrika Kusini katika kijiji cha Ihemi mahali ambapo kitajengwa chuo hicho.
Viongozi hao wakilitazama eneo hilo kwa upande wa pili wa barabara kuu ya Iringa- Mbeya- Tunduma.
Kutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Asha Rose Migiro na Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Chrstine Ishengoma pamoja na wageni wengine wakiwa katika ukumbi wa mkutano Kambi ya Ihemi.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM kulia akisalimiana na Lucas Kisasa aliyewahi kuwa mhariri Mkuu wa Uhuru Publication.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM akionyesha eneo hilo kwa upande wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya.
Wakiendelea kutathmaini eneo hilo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Emanuel Mteming'ombe akiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa vijana wa mkoa wa Iringa Ahmed Asas.
0 comments:
Post a Comment