SERIKALI imesema leseni nyingi zinazotumika
katika shughuli za utalii ni feki wengi
wao wakiwa na simu za mikononi peke yake huku makazi na sehemu za kufanyia
shughuli hizo kutokuwepo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis
Kagasheki alisema hayo jana Dar es salaam wakati akizundua bodi ya leseni ya
bishara za utalii, mamlaka za rufaa wizarani hapo na Kamati ya ushauri.
Kuhusu leseni feki aliomba kupatiwa orodha ya
wanaohusika na shughuli hizo kwani wengi wana leseni ambazo
ni batili kutokana na utaratibu
wa upatikanaji wake kutoeleweka.
“Katika wale wanaojishughulisha na biashara hiyo
wengi wana simu za mikononi tu, huku makazi na sehemu za biashara kutokuwepo lakini wanapewa leseni,” alisema
Balozi Kagasheki na kuongeza kuwa sekta hiyo ina umuhimu wa pekee na haijulikani wanazipateje leseni hizo na inaonesha
wanapewa kinyume na utaratibu.
Aidha alisema serikali itaanza msako kuhusiana
na hilo ili kuwe na njia za kudhibiti
hao ambao huchukua mapato kinyume na utaratibu unaotakiwa ili kuziba mianya
hiyo na kuifanya biashara ya utalii kuwa nzuri huku akiagiza Bodi
zilizozinduliwa kushughulikia suala hilo ambalo hupoteza mapato mengi.
Akizungumza kuhusu masuala ambayo Bodi hizo zinapaswa
kuyashughulikia kwa haraka alisema ni pamoja na kutizama kwa haraka suala la
uboreshaji wa sera ya utalii ili kwamba iweze kuwa na sura y akitaifa na
kimataifa kulingana na wakati uliopo.
“Ni vyema mkatizama sera imeekaje vilevile na
sheria ya utalii ya mwaka 2008 kwani inaonekana kana kwamba wanasheria
waliitunga kwa haraka haraha kutokana na kuwa na mikanganyiko mingi,” alisema
Balozi Kagasheki.
Aidha alitoa mfano Makumbusho ya Taifa ambapo
sheria yake ni ya mwaka 1980 ambapo hadi sasa hakuna kanuni jambo
linalosababisha utekelezaji wa sheria hizo kutotelekezeka.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi hizo wakifuatilia hotuba hiyo ya uzinduzi kutoka kwa Waziri.
Wajumbe wa bodi ya Leseni katika picha ya Waziri.
Wajumbe wa kamati ya Ushauri.
wajumbe wa Kamati ya rufani
Baadhi ya wajumbe wa Mamlaka ya Rufani,
Crescencia Rwechungura (katikati), Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri, Dk.
Wineaster Anderson pamoja na mjumbe wa bodi ya Leseni, Scholastica Ponera
wakijadiliana jambo nje ya ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Utalii na Maliasili
Dar es Salaam jana mara baada ya kuzindiliwa kwa bodi hizo.
0 comments:
Post a Comment