Mtafiti Mkuu na Mkurugenzi wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano kutoka Taasisi ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Bw. Leonard Mboera(kulia) akieleza kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu Mifumo mbalimbali ya utoaji taarifa
za Tafiti zinazofanywa na Taasisi hiyo,wakati wa mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa
Hbari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Frank Mvungi.
UTANGULIZI
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu ilianzishwa kwa sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Namba 23 ya mwaka 1979. Makao makuu ya Taasisi yako Dar es Salaam. Taasisi ina
vituo vikuu saba (Amani, Mbeya, Muhimbili, Mwanza, Tabora, Tanga, Tukuyu na
Ngongongare) na vituo vidogo saba (Amani Hill, Gonja, Handeni, Haydom, Kilosa
na Korogwe).
Majukumu ya Taasisi
1. Kuratibu, kukuza na kuendeleza utafiti wa
afya Tanzania
2. Kufanya utafiti wa afya ili kupunguza
magonjwa yanayosumbua jamii ya Watanzania
3. Kufaya utafiti wa tiba asilia na tiba mbadala
4. Kusajili tafiti za afya zinazofanywa nchini
5. Kuwapa uwezo Watanzania katika kufaya tatifi
wa afya
6. Kukuza matumizi ya matokeo ya tafiti za afya
Taratibu za Kitafiti
Mzunguko mzima wa utafiti unahusisha mambo
yafuatayo:
1. Maandalizi ya Rasimu
2. Maombi ya Kibali cha Kufanya Utafiti
kinachozingatia maadili ya utafiti unaojumuisha binadamu
3. Maandalizi ya Utafiti
4. Ukusanyaji wa takwimu
5. Menejimenti ya takwimu na mchanganuo wake
6. Matayarisho ya Taarifa ya Utafiti
7. Uwasilishaji wa matokeo kwa wadau mbalimbali
(Mikutano, Warsha, Kongamano, Tovuti)
8. Uchapishaji wa Taarifa ya Utafiti katika
Ripoti na Majarida ya Sayansi
9. Uandaaji wa muhtasari wa utafiti kwa ajili ya
sera na uboreshaji wa utendaji
0 comments:
Post a Comment