Nafasi Ya Matangazo

October 31, 2013

 Pichani kulia ni Innocent Melleck Mratibu Uhuru marathon,akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,mapema jana ndani ya Idara ya HABARI MAELEZO,kuhusiana na kutangaza rasmi utoaji fomu za usajili kwa ajili ya mbio hizo jijini Dar es Salaam, ambapo vituo zaidi ya 13 vilivyofunguliwa katika maeneo mbalimbali.
Innocent Melleck aliongeza kuwa  pia siku ya Jumanne na Jumatano wiki ijayo, fomu hizo zitatolewa rasmi katika Viwanja vya Bunge, Dodoma ambapo Mheshimiwa Spika Anne Makinda ndiye anayetarajiwa kuongoza katika kujisajili, pia katika usajaili huo amewaomba waheshimiwa wabunge wajiandae na wajitokeze kwa wingi ili kulifanikisha zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa. 
 Melleck akizungumza mbele ya Wanahabari
Melleck akionesha fomu za usajili kwa ajili ya shindano hilo,mbele ya wanahabari (hawapo pichani),aidha ameongeza kuwa anayetaka kushiriki anaweza pia kujisali kwa njia ya mitandao ya kijamii kama www.uhurumarathon.com,  issamichuzi.blogspot.com,jiachie Blog,mtaa kwa mtaa Blog,Father  kidevu.blogspot.com,kajunason.Blog,weyunga.blogspot.com na nyingine nyiingi.

Katika usajili huo, fomu zitakazotolewa zitauzwa kwa bei ifuatayo; kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipia Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.
"Kama ambavyo tumezungumza awali kuwa kesho zoezi hili linaanza rasmi kwa fomu kuanza kuuzwa na leo hii nawajulisha Watanzania wenzangu kuwa fomu namba moja ya mbio za Km3 itakuwa maalumu kwa Rais Dr.Jakaya Kikwete,ambae amekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha watanzania kutambua kwa vitendo umuhimu wa kuenzi umoja,mshikamano na amani iliyopo pasipo kujali itakadi zozote zile,

Pia spika wa bunge letu tukufu Anna makinda yeye atachukua fomu namba mbili ,fomu namba tatu itapelekwa kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA na mkuu wa kambi rasmi ya upinzania bungeni na fomu nyingine hadi fomu namba 100 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wetu mbalimbali wa vyama vya kisiasa, viongozi wa dini zote na viongozi wa serikali na mashirika binasi",aliseme Melleck.
Posted by MROKI On Thursday, October 31, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo