Mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala,Dar es
Salaam City College(DACICO)Faudhia Hassan,akipiga kura wakati wa zoezi
la kuwachaguaViongozi wa Serikali ya wanafunzi kwa nafasi za Rais wa
Chuo na Nafasi ya Makamu.
Uchaguzi huo Umefanyika Makao Makuu ya Chuo, Kibamba Dar es Salaam leo.
Mmoja
wa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala,Dar es Salaam
City College(DACICO)Rehema Mussa,akipiga kura wakati wa zoezi la
kuwachaguaViongozi wa Serikali ya wanafunzi kwa nafasi za Rais wa Chuo
na Nafasi ya Makamu. Uchaguzi huo Umefanyika Makao Makuu ya Chuo,
Kibamba Dar es Salaam leo.(Picha Deogratius Peter).
Na, William Severine,Mathias Maule, Grace George wa DACICO.
Wanafunzi
wa Chuo cha Dar es Salaam City College kilichopo jijini dar es salaam
manispaa ya kinondoni, leo wamefanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wao
katika nafasi ya urais na makamu wa rais kutokana na uongozi uliopo
madarakani kumaliza muda wao ,
Wakizungumzia tukio hilo kwa nyakati tofauti,baadhi ya wanafunzi
walisema kuwa tukio hilo limechukua muda mrefu sana kufikia uchaguzi
huo kutokana na kuairishwa kwa tarehe ya mwanzo ambayo ulipangwa
kufanyika October 22 mwaka huu. Mwenyekiti wa Tume ya kamati ya
kusimamia Uchaguzi huo Mussa Moses alisema kuwa sababu za kusogezwa
mbele ni kutokana na tume kutokuwa makini na kile kilichoelezwa kuwa ni
kuruhusu uongozi wa juu wa chuo kuingilia maamuzi yao kama tume ya
uchaguzi.
Hata hivyo mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi ndugu musa moses
alipinga tuhuma hizo na kusema kuwa tume haikuingiliwa katika maamuzi
yake bali walikubali maombi yaliyo toka uongozi wa juu wa chuo ya
kuomba kuuboresha uchaguzi huo na kuomba ufanyika October 30 mwaka huu
.Pia mmoja wa wagombea hao katika nafasi ya urais ndugu, Mathias Canal
alisema anashukuru hatua ambayo chuo kimefikia cha kufanya uchaguzi huru
na kutoa pongezi zake kwa tume ya uchaguzi kwa kufanikisha zoezi hilo.
Wagombea
waliojitokeza katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Mathias
Canal,Hilary Mgenzi,Christopher Mwakasanga(Urais) na kwa nafasi ya
Makamu wa Urais ni pamoja na Razack Mushi, Mathias Haule, na Rozalina
Mchomvu.
Aidha mkurugenzi wa chuo mr. idrisa mziray alitoa pongezi kwa wanafunzi
wote kwa kujitokeza na kushiriki katika tukio hilo la upigaji kura
kutoka na kuwa ni haki yao ya kimsingi ili kujipatia viongozi walio bora
kwa maslai yao na chuo kwa ujumla.
"
Uchaguzi Umekwenda Vizuri, kikubwa nawapongeza wanafunzi wote kwanza kwa
kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura, pia nawapongeza wasimamizi kwa
kuandaa Uchaguzi huru na wa haki maana wametimiza misingi ya
Demokrasia, hakuna malalamiko kutoka pande zote, hili ni jambo la
kujivunia sana, kwa kuwa chaguzi nyingi vyuoni uambatana na vurugu na
pia Rushwa za hapa na pale" alisema Mziray
Matokeo ya Uchaguzi huo yanatazamiwa kutangazwa mapema kesho baada ya kuhesabiwa na wasimamizi wa Tume ya Uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment