MNAMO Mwezi Agosti mwaka huu,
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe alitoa miezi mitatu kwa watu wote
walioingiza matrekta nchini ya kifungu cha msamaha wa kodi ili kuboresha kilimo
nchini, wahakikishe zana hizo zinatumika kwa kazi hiyo na siyo vinginevyo.
Dkt. Mwakyembe alitoa agizo
hilo wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya wakulima kwa nyanda za juu kusini katika
Viwanja vya John Mwakangale, huku akiagiza tabia ya kutumia matrekta kubeba na
kukokota mizigo bandarini ikomeshwe mara moja na matrekta hayo yapelekwe
mashambani kwa ajili ya kilimo.
Lakini wakati leo ndio miezi
mitatu imetimia tangu agizo hilo litolewe na Waziri huyo mwenye makeke mengi
katika utendaji wake wa kazi kiasi cha kuleta ufanisi katika taasisi zilizo
chini yake kama bandari na Viwanja vya ndege nchini, inaonesha dhahiri kupuuzwa.
Father Kidevu Blog, inatumia
fursa hii kumkumbusha Waziri huyo kuwa agizo lake halijafanyiwa kazi na
matrekta hayo yapo na yanaendelea kupeta pasi na shaka katika kubeba mizigo
bandarini hata kusafirisha taka kutoka katikati ya mji hadi katika madampo nje
ya miji hasa Pugu Kinyamwezi.
0 comments:
Post a Comment