Baada ya usaili wa kumtafuta mrembo wa kurithi
taji la Miss Universe Tanzania kumalizika, kambi ya warembo kwa ajili ya
kinyang’anyiro cha kumtafuta mrithi wa taji la Miss Universe Tanzania 2013
imeanza rasmi.
Kambi hii ambayo imejumuisha warembo 15 kutoka
mikoa nane ya Tanzania itakaa kwa muda wa wiki moja katika hotel ya Urban
Rose kabla ya kumpata mshindi siku ya fainali ambapo itakuwa tarehe 27
mwezi Septemba mwaka huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Ukilinganisha na miaka mingine mashindano ya mwaka
huu yatakuwa tofauti kidogo ambapo ukiondoa kugombania taji kubwa la Miss
Universe Tanzania kulikuwa na washindi wa pili na watatu. Mwaka huu mshindi
mwingine atavikwa moja kwa moja taji la Miss Earth Tanzania na Mshindi wa tatu
bora ndio atakua runner up. Warembo watakaochuana kuwania taji hilo ni kama
ifuatavyo na mikoa waliyotoka kwenye mabano.
Aziza
Victoria(Dar es Salaam) , Irene Nsiima (Dar es Salaam), Betty Boniface(Dar es
Salaam), Kundi Mlingwa(Dar es Salaam), Mariam Ngwangwa(Dar es Salaam) , Consolata
Mosha( Mwanza), Agnes Thobias, Dinah David ( mbeya), Upendo Dickson (Dar es
Salaam), Naomi Kisaka(Dar es Salaam), Glady Msemo(Dar es Salaam) , Vestina
Mhagama(Dar es Salaam) , Angela Lutataza(Dar es Salaam) , Clara Noor( Mwanza),
Sasha Lukiko(Dar es Salaam).
Timu ya Compass Communications ilizunguka
takriban Mikoa 8 ya Tanzania kufanya usahili kwa kila mkoa ili kupata
wawakilishi wa mikoani katika kinyang’anyiro hiki. Mikoa hiyo ni pamoja na
Mwanza, Arusha, Mtwara, Manyara, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Jumla ya washiriki 15 wataingia kambini kuchuana kumpata Mwakilishi wa Tanzania
katika fainali za dunia zitakazofanyika nchini Moscow,Urusi.
Mashindano ya Miss Universe kwa hapa Tanzania
yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo Tanzania iliwakilishwa na Flaviana Matata na
kufanikiwa kuingia katika kumi bora na mwaka 2008 yaliwakilishwa na Amanda Ole
Sulul, 2009 yaliwakilishwa na Illuminata James ambapo mwaka 2010 mrembo Hellen
Dausen ndiye aliyepokea kijiti, 2011 Nelly Alexandra Kamwelu na anayekabidhi
taji mwaka 2012/2013 ni Winfrida Dominique.
Mashindano ya Miss Universe yamedhaminiwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA), Fastjet, Mohamed Enterprises (MetL) na Wadhamini wenza(Parters) ni CocaCola, Missie Popular Blog, Healthy
Beauty Clinic, Beauty Point, Sia Couture, Seif Kabelele Blog, AZH
Photography.com na Adams Digicom
0 comments:
Post a Comment